Jonas Kamaleki-MAELEZO
Chama cha Labour cha nchini
Uingereza kimepongeza juhudi za Rais John Pombe Magufuli na Serikali
yake kwa utendaji mzuri katika kulinda na kugawanya rasilimali kwa watu
wake.
Pongezi hizo zimetolewa hivi
karibuni na Viongozi wa Labour Party katika Mkutano na vyama mbali mbali
vya kisiasa vikiwemo vya...
Kiafrika vya SWAPO, ANC na CCM, uliofanyika
Uingereza kama anavyoeleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa kimataifa,
Kanali (Mstaafu) Ngemela Lubinga katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.
“Chama cha Labour kinataka haki
sawa kwa wote, kwa hiyo kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kusimamia rasilimali na kuhakikisha
rasilimali zetu zinazoibiwa zisiibiwe tena, kimewapa faraja,” alisema
Lubinga.
Lubinga amesema kuwa Serikali ya
Awamu ya Tano inasimamia rasilimali kitendp ambacho kitaleta maandeleo
kwani hakuna maendelo yanyowezakupatikana bila usimamizi wa rasilimali.
“Chama cha Labour kinapigana
kuhakikisha wananchi wake wanapata makazi bora, hivyo suala la Accacia
ambao walikuwa wakifanya vitendo visivyoendana na hali halisi ya
rasilimali hasa kwetu sisi walengwa kimewafurahisha sana na kuona kuwa
mazungumzo yamekamilika katika mazingira ya kukubaliana namna ya
rasilimali hizo zinavyotumika kuwanufaisha watanzania,”alisema Lubinga.
Kuhusu mwelekeo wa uchumi, Kanali
(Mstaafu) Lubinga amesema kuwa uchumi wa Tanzania unakua na utakuwa wa
kuvutia kwani juhudi za makusudi zinafanyika hivyo amewataka wanachi
wawe na subira.
Ameongeza kuwa wazazi wawaandae
watoto wao kufanyakazi na wasiwaachie tu kwenda wanavyotaka. Ametoa
mfano kuwa mtu akiona mtoto wake amenunua gari la kifahari inabidi
amuulize fedha ametoa wapi za kununua gari hilo wakati mshahara wake
unajulikana na ni mdogo.
Amewataka watanzania wawe
wavumilivu kwani mabadiliko huleta kiwewe kwa wat na yakishaleta matokeo
chanya, watu hao husahau walioleta maendeleo hayo.
Serikali ya Awamu ya Tano
imetimiza miaka miwili tangu iingie madarakani tarehe 5 Novemba, 2015.
Katika kipindi hiki watanzania wameshuhudia miradi mikubwa ya maendeleo
ikianzishwa na kutekelezwa, mfano ujenzi wa barabara,madaraja, ununuzi
wa ndege sita, ujenzi wa reli ya kisasa, (standard gauge), utengenezaji
wa madawati na elimu bure kwa elimu ya msingi na mwisho nidhamu ya kazi
imerejea katika utumishi wa umma.
No comments :
Post a Comment