Wednesday, November 8, 2017

BALOZI SEIF AZITEMBELEA FAMILIA ZILIZOATHIRIWA NA MAFURIKO SHEHIA YA BUBUBU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifanya ziara ya kukagua maeneo yaliyoathirika na Mvua za Vuli katika Shehia ya Kijichi Wilaya ya Magharibi”A”.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Kepteni Khatib Khamis wa kwanza kutoka Kushoto akimpatia maeleza Balozi Seif juu ya maafa ya mabvua za Masika zilizoathiri Shehia ya Jikichi.
Balozi Seif akiuagiza Uongozi wa Wilaya ya Magharibi A kusimamia sheria na taratibu dhidi ya watu wanaoamua kujenga bila ya kuzingatia Sheria zilizowekwa.
Kasi ya maji ya mvua yanayoonekana yakititirika katika Mto wa Bububu kutokana na baadhi ya Watu wengi kutozingatia njia za maji hayo kutokana na ujenzi holela.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizipa pole Fmilia mbili zilizooondokewa na Jamaa zao kufuatia mafuriko ya mvua za Vuli zilizonyesha Juzi.

Wa kwanza kutoka Kulia ni Bwana Hussein Khamis aliyevaa Fulana rangi ya Kijani aliyefiwa na Mama yake Mzazi Marehemu Bibi Salma Khamis na Bwana Rajab Moh’d aliyefiwa na Mtoto wake. Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments :

Post a Comment