Friday, October 20, 2017

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AWATAKA WAFANYAKAZI MIZANI KUACHA RUSHWA.



Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa, akiangalia namna watumishi wa mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga wanavyopima na kurekodi taarifa za magari yanaoingia kupima uzito kwenye mzani huo.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (Mwenye suti), akiangalia namna shughuli za upimaji wa magari zinavyoendeshwa katika mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga. Kushoto kwake ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wa mkoa huo, Mhandisi Mibala Ndilindi.


Msimamizi wa shughuli za mzani wa Tinde kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Shinyanga, Bw. Lugembe Vicent (kushoto), akitoa taarifa ya kiutendaji ya mzani huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa. Mzani huo unapima magari 300 kwa siku.


Magari yakiwa katika foleni kusubiri huduma za upimaji uzito ili kuendelea na safari kwenye mzani wa Tinde, mkoani Shinyanga.



NA WUUM, SHINYANGA
WAFANYAKAZI wa mizani nchini wametakiwa kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuachana na vitendo vya rushwa ili kuleta tija na ufanisi wa kazi zao
katika usimamiaji na ulinzi wa barabara ambazo Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika ujenzi wake.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa, leo mkoani Shinyanga, alipokuwa akikagua  mzani wa Tinde (Shinyanga), na Mwendakulima (Kahama),  ambapo amesisitiza ushirikiano kati ya wafanyakazi hao na madereva ili kutatua changamoto zinazojitokeza katika  vituo vya mizani.

No comments :

Post a Comment