Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Koplo
Faustina Ndunguru kutoka Makao Makuu ya Trafiki kitengo cha Elimu ya
Usalama Barabarani katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa
ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira (kushoto) na Kulia ni Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Usalama barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Fortunatus Musilimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa
Usalama na Mazingira kutoka TANROADS Makao Makuu Bi. Zafarani Madayi
wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho yanayotoa elimu ya usalama
barabarani katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa ya Moshi
mjini mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Msaidizi Usalama na
Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Joyce Mbunju
akimuelezea Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan namna Wizara ilivyojipanga
nakuja na mbinu za teknolojia ya kisasa katika kuhakikisha usalama
barabarani unakuwepo wakati wote.
Mwanafunzi wa Darasa la 5 kutoka
shule ya msingi Muungano Bi. Aisha Ayoub akishiriki kuima nyimbo za
kuelimisha masuala ya usalama barabarani akiwa mmoja kati ya wanafunzi
waliotoka shule 10 za Manispaa ya Moshi mjini wakati wa uzinduzi wa wiki
ya nenda kwa usalama barabarani ambao umefanyika katika viwanja vya
Mashujaa ambapo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni
rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa ,Manispaa ya Moshi mjini
mkoani Kilimanjaro.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments :
Post a Comment