Friday, September 29, 2017

WAZIRI LWENGE AZINDUA BODI MPYA YA MAJI YA BONDE LA ZIWA TANGANYIKA MKOANI KIGOMA


048A1721
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akizindua jengo jipya la Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Tanganyika na Maabara ya Maji

048A1663Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akitia saini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa waKigoma. Pembeni yake ni Kaimu Mkuu wa MkoaNdugu Samson Anga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma.
048A1699
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi kitendea kazi Mwenyekiti w aBodi mpya aliyoizindua ndugu Lister Kongola.
048A1726Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na Bodi mpya ya Maji ya Bonde la Ziwa Tanganyika na viongozi wengine.
048A1768Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akipewa maelezo ya kuhusu mradi na Mhandisi Mshauri wa mradi Mhandisi Michael Mwamu kinga wakati akikagua mradi wa maji.Kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ndugu Samson Anga.
……………………..
Waziri wa Majina na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge amezindua Bodi mpya ya Maji ya Bonde la Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma Septemba 28, 2017 na kuitaka Bodi hiyo kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za maji zilizopo ndani ya bonde hio kwa matumizi endelevu.
“Bonde la Ziwa Tanganyika ni bonde la tatu kwa ukubwa katika mabonde tisa yaliyopo nchini ambapo mabonde 7 ni shirikishi.
 Alisema bonde hili ni shirikishi na nchi za DRC-Congo, Burundi, Rwanda na Zambia.
"Asilimia 60 ya maji yanayoingia katika Ziwa Tanganyika yanatoka Tanzania hivyo bonde hili kwa Tanzania tunalitegemea sana." Alisema.
Mhandisi Lwenge alisema, sababu ya kuundwa kwa Bodi ni utekelezaji wa sheria ya Maji No. 11 ya Mwaka 2009 na Bodi itasimamia matumizi endelevu ya rasilimali za maji.
“Bodi hii ni muhimu sana kwa hiyo kuteuliwa kwenu isiwe ni kwenda kupata posho tu na kutowajibika ipasavyo bali ni kufanya kazi tunayoitegemea ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi” alisemaWaziri.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi amesema bodi yake itatekeleza maagizo yote ya Mhe. Waziri.

No comments :

Post a Comment