Kushoto, Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kulia ni Mwenyeji
wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe katika kikao
kabla ya kuanza ziara ya ukaguzi wa viwanda Mkoani hum oleo.
Kushoto kaimu mkurugenzi wa
mamlaka ya maji safi na maji Taka mjini Mororgoro, inginia Halima Mbiru,
akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Mpaka wa mabwawa ya maji taka mali ya
mamlaka hiyo, hayapo katika picha. Mhe. Mpina alifanya ziara ya ukaguzi
wa mabwawa hayo mapema leo.
Katikati Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Mbele yake ni
Bw. George Mratibu wa Kiwanda cha Ngozi Morogoro , cha ACE LATHER
TANZANIA LTD, wakiwa katika ukaguzi wa mtambo wa kisasa wa kutibu
majitaka kiwandani hapo ambapo Mpina yupo Mkoani Morogoro katika ziara
ya ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria ya Mazingira na kanuni zake,
kufuatia maagizo aliyoatoa awali katika ziara ya viwanda hivyo.
Katika picha ni washiriki katika ziara ya Naibu Waziri Mpina alipokagua Mabwawa ya majitaka kama yanavyoonekana katika picha.
Picha na Evelyn Mkokoi
…………….
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,
Luhaga Mpina Amekipongeza kiwanda cha nguo cha 21st century na kiwanda
cha ngozi cha ACE LEATHER TANZANIA LTD kwa kutekeleza sheria ya
...mazingira kwa kujenga mtambo wa kisasa wa kutibu majitaka yanayotoka
katika viwanda hivyo.
Akiwa katika Ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa Sheria ya
mazingira Mkoani Morogoro leo, Mpina aliwataka wamiliki wa viwanda hivyo
kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira NEMC pamoja na Bonde la Wami Ruvu, kuchukua Sampuli za maji
hayo yanayotibiwa katika viwanda hivyo kwa ajili ya vipimo ili
kujiridhisha kuwa hayana madhara kwa mazingira na viumbe hai wengine.
Naibu Waziri Mpina anaendela na ziara yake ya ukaguzi wa mazingira na utekelezaaji wa shieria ya mazingira mkoani Morogoro.
No comments :
Post a Comment