Meneja Mkuu wa Ksmpuni ya
Linghang,Cathy Wang kutoka jiji la Shanghai China walipotembelea Ofisi
ya Meya wa Dar es salaam Isaya Mwita.
Meya wa Jiji la Dar es salaam
Isaya Mwita akiwa na wageni kutoka China walipomtembela Ofisini kwake
wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wageni kutoka jiji la Shanghai
nchini China wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionesha bendera ya
Taifa la nchi yao walipotembelea Ofisi ya Meya wa Dar es salaam.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwa katika picha ya pamoja.
PICHA NA ALEX SONNA WA FULLSHANGWEBLOG.
…………………….
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es
Salaam, Isaya Mwita amekutana na ugeni kutoka Jiji la Shanghai nchini
China na kujadili mambo mbalimbali ya ...maendeleo jijini hapa ikiwemo
suala la uboreshaji wa Kituo cha Mabasi Ubungo.
Ugeni huo uliambatana na Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Linghang Group, Cathy Wang ambayo imeingia mkataba na
halmashauri ya jiji kwa ujenzi wa kituo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo, Meya Mwita
alisema kuwa ugeni huo umeridhia kuwekeza katika nyanja mbalimbali
ikiwemo Kituo cha Mabasi Ubungo.
Alifafanua kuwa Jiji la Dar es
Salaam linakaribia kuanza kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa kubadilisha
Kituo cha Mabasi Ubungo na kwamba hatua mbalimbali zimeshakamilika ili
kupisha mradi huo.
Alisema kuwa mara baada ya
kukamilika kwa mradi huo jumla ya Watanzania 20,000 watapata ajira jambo
ambalo litawezesha kuongeza kipato kwa wananchi na hivyo pia kuwezesha
vijana kuondokana kwenye makundi ambayo sio salama.
Alisema kufanikishwa kwa mradi
huo, utasaidia pia kuongeza mzunguko wa fedha jijini hapa kutokana na
kuwepo kwa fursa nyingi za kibiashara.
“Leo nimekutana na ugeni ambapo
kwa kiasi kikubwa mnafahamu ndugu zetu hawa wamekuwa na urafiki mkubwa
katika nchini yetu, tumejadiliana mambo mengi ambayo yote ni ya kuleta
maendeleo katika jiji letu.
“Lakini kubwa zaidi ni kuhusu
ujenzi wa Kituo cha Mabasi Ubungo, ambapo hivi karibuni tunatarajia
kuanza kwa mradi huo, na wananchi pia watajulishwa, nitumie fursa hii
kuwaeleza wananchi kuwa jiji linafuata utaratibu katika kutekeleza mradi
huo,” alisema Meya Mwita.
“ Fursa hii ni kubwa ambayo
tumeipata, Watanzania watapata ajira, mzunguko wa fedha kwenye jiji letu
utaongezeka, kama meya wa jiji hili nimewakaribisha tufanye kazi
pamoja, lengo likiwa ni kuweka jiji kwenye muonekano mzuri,” aliongeza.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa
Kampuni ya Linghang, Cathy Wang alimpongeza Meya Mwita kutokana na aina
ya utendaji wake wa kazi na kuahidi kuonyesha ushirikiano katika
utekelezaji wa mradi huo.
Alisema kuwa Meya Mwita ni
kiongozi anayefanya kazi kwa bidii na umakini na kwamba kutokana na
jitihada hizo za kulijenga jiji , kampuni yao itafanya kazi na
kumhakikishia kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
No comments :
Post a Comment