Pages
Saturday, September 9, 2017
TPSF YAMWAGA BALOZI WA CHINA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)
imeagana na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing
katika hafla fupi ambayo imefanyika katika hoteli ya Serena iliyopo Dar
es Salaam.
Akizungumza katika hafla ya kumuaga, Mwenyekiti wa TPSF, Dk. Reginald
Mengi alimshukuru Dk. Youqing kwa mambo yote ambayo ameyafanya akiwa
balozi wa China nchini na kumuomba kuendelea kushirikiana na Tanzania
hata atakaporejea China.
“Muda mwingine nashindwa kujua kama unaiwakilisha China au Tanzania
umekuwa na matendo mema kwa Tanzania kwa kipindi chote ambacho umefanya
kazi nchini umekuwa daraja kubwa la kuunganisha China na Tanzania,
“Wote tunajua umuhimu wa biashara ya Tanzanania na China ilivyo kubwa na
mambo mambo mengi uliyoyafanya yalifanikiwa, jambo ambalo tunaweza
kusema ni tutakukumbuka sana,” alisema Dk. Mengi.
Kwa upande wa Dkt. Lu Youqing aliishukuru (TPSF kwa ushirikiano waliomba
kwa kipindi chote ambacho alikuwa akifanyakazi nchini na kuahidi kuwa
hata atakaporudi China ataendelea kushirikiana nao.
“Tumeishi vizuri kwa kipindi nilichokuwa hapa niwaahidi kuwa nitarudi
tena Tanzania nikiwa kama mfanyabiashara na siku moja ninapenda kuwa
mwanachama wa TPSF, kuweni huru kuja hata China kujifunza namna China
tunafanya biashara,”alisema Dkt. Youqing.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi
akisalimia na Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu
Youqing. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na
Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiingia
katika ukumbi wa mikutano wa Kivukoni uliopo katika hoteli ya Serena,
Dar es Salaam. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi
akizungumza katika hafla ya kumuaga Balozi wa China aliyemaliza muda
wake chini Dkt. Lu Youqing. Balozi
wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing akizungumza katika
hafla ya kumuaga baada ya muda wake wa kufanya kazi nchini kuisha. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na
Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiwa na
viongozi wengine wa TPSF walioshiriki hafla ya kumuaga Balozi Youqing. Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi na
Balozi wa China aliyemaliza muda wake chini Dkt. Lu Youqing wakiwa
kwenye picha ya pamoja na viongozi wa TPSF.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment