Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Louiza
Shem akitoa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya moyo wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya
Taasisi hiyo. Pamoja na kutoa elimu ya afya bora Taasisi hiyo imetoa huduma ya
upimaji afya bila malipo na kutoa dawa bila malipo kwa kushirikiana na
makampuni yanayotengeneza dawa za binadamu na Shirikisho la Magonjwa yasiyo
kuwa ya Kuambukiza (TANCDA).
Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Mary Haule akimpima sukari Charlote Guzuye mkazi wa
Kinyerezi jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo
Duniani yaliyofanyika leo. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure
magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa bure na
kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Waandishi wa Habari wa kituo cha Televisheni cha Tumaini wakifanya
mahojiano na bibi Lena Mwambija mkazi wa Kinyerezi jijini Dar Es Salaam
aliyefika katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo bila malipo ikiwa ni siku ya
Maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani.
Afisa Muuguzi kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lucy Nyawike akimpima shinikizo la
damu (BP) Mwandishi wa Habari wa kituo cha Televisheni cha Clouds
Rachel Chizoza wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani
yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya
upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa
dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aloyce Mohamed akimkabidhi dawa za ugonjwa wa moyo
Abdala Shomvi mkazi wa Mkuranga Mkoani Pwani wakati wa maadhimisho
ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo
licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa
na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya
bora ya Moyo.
Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Lucia Kabeya akimpima msukumo wa damu (BP) Subir
wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini
Dar es Salaam. Taasisi hiyo licha ya kutoa huduma ya upimaji bure magonjwa ya
moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za moyo bure na kupewa
elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hania
Bwahama akimpima sukari Shabani Juma wakati wa maadhimisho ya siku
ya Moyo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo kwa
kushirikiana na baadhi ya makampuni ya dawa na chama ilitoa upimaji
bure magonjwa ya moyo pia wagonjwa waliokutwa na matatizo walipatiwa dawa za
moyo bure na kupewa elimu ya lishe bora kwa afya bora ya Moyo.
Wananchi wakisubiri kupata huduma ya upimaji
magonjwa ya moyo bure wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani
yaliyofanyika leo katika viwanja vya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar
es Salaam.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Lugendo
akimpima shinikizo la damu (BP) Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamini
Mkapa Leyla Faiz wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani
yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo elimu ya lishe bora kwa
afya bora ya Moyo na kutoa dawa bila malipo kwa kushirikiana na makampuni
yanayotengeneza dawa za binadamu na Shirikisho la Magonjwa yasiyo kuwa ya
Kuambukiza (TANCDA).









No comments :
Post a Comment