Monday, September 4, 2017

JAMII YA KIFUGAJI YAPEWA ELIMU JUU YA UFUGAJI NYUKI

Mkufunzi wa mafunzo ya ufugaji nyuki Baltazar Lylimo akitoa maelezo kikundi kilichopo
kijiji cha Ketumbeini,Wilaya Longido Mkoani Arusha kuhusu namna mizinga inavyoweza kuhifadhi Asali nyingi endapo watafuata maelekezo ya ufugaji,Kulia ni Mkuu wa Jimbo la Kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania(KKKT)Dayosisi ya kaskazinikati jimbo la Arusha Magharibi Mch.Isaac Kisiri(Picha na Pamela Mollel Arusha)
 
Wanakikundi wakishuhudia mzinga wa nyuki ukiwa juu ya mti mara baada ya kufundishwa njia bora ya ufugaji nyuki katika kijiji cha Ketumbaine
Wilayani Longido Mkoani Arusha,

Mkuu wa Jimbo la Kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania(KKKT)Dayosisi
ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Mch.Isaac Kisiri akizungumza na viongozi wa kikundi cha ufugaji nyuki

Mratibu wa miradi ya kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania(KKKT)Dayosisi
ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Simon
Sandilen akizungumza na vyombo vya habari juu ya semina ya ufugaji nyuki
Wanakikundi wakishuhudia mzinga wa nyuki ukiwa juu ya mti mara baada ya kufundishwa njia bora ya ufugaji nyuki katika kijiji cha Ketumbaine
Wilayani Longido Mkoani Arusha,
Mkuu wa Jimbo la Kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania(KKKT)Dayosisi
ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Mch.Isaac Kisiri akizungumza faida za ufugaji nyuki


Mkufunzi wa semina juu ya ufugaji nyuki, Baltazar Lyimo kusoto akiwaonyesha wanakikundi vazi maalumu la kuvaa wakati wa uvunaji asali

Muonekano wa eneo hilo katika picha
          Jengo la kanisa
  Picha ya pamoja baada ya semina ya ufugaji nyuki

Zaidi ya
wanakikiundi 150 katika kijiji cha Ketumbaine Wilayani Longido Mkoani Arusha,wamepatia
semina ya ufugaji nyuki itakayowasaidia kujipatia kipato sambamba na chakula
Akizungumza
na waandishi wa habari hivi karibuni 
Mratibu wa miradi ya kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania(KKKT)Dayosisi
ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi
Simon Sandilen alisema kuwa
mradi huo unathamani ya shilingi Milioni
tatu 
 
Alisema kuwa Asali
mbali na kutumiwa kama chakula pia hutumika kama dawa hivyo ni vyema
wanakikundi wakafundishwa njia za kisasa za ufugaji nyuki ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na umasikini
 
Hata hivyo
alisema kuwa jamii hiyo ya kimaasai itaweza kunufaika na semina hiyo ya siku
moja kwa kujua mbinu zitakazowawezesha kuwaongezea kipato kwa muda mfupi
ukilinganisha na miradi mingine
Kwa upande
wake
Mkuu wa Jimbo la Kanisa la kiinjili la KilutheriTanzania(KKKT)Dayosisi
ya kaskazini kati jimbo la Arusha Magharibi Mch.Isaac Kisiri
  alisema
kuwa mradi huo umefadhiliwa na kanisa la kilutheri la huko  Ujerumani
Alisema kuwa
mradi huu utasimamiwa kikamilifu pamoja na miradi mingine itaendelea vizuri na
italeta matokeo mazuri yaliyokusudiwa kwa kuwa uongozi unaosimamia hiyo miradi
upo imara
Mnufaika wa
semina hiyo ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Joseph Ndila alishukuru
kwa semina hiyo huku akisema elimu waliyoipata wataweza kuwaelimisha na
wafugaji wengine
“Aliongeza
kuwa ufugaji wa awali haukuwa wa  kisasa
kwakuwa walikuwa wakiua nyuki bila sababu lakini leo tumefundishwa njia sahihi
za kurina asali na vifaa muhimu vya kutumia katika uvunaji asali”alisema Ndila
Naye
Mkufunzi wa semina hiyo Baltazar Lyimo alisema kuwa wananchi wa eneo hilo
wanarasilimali miti ambayo itawawezesha wafugaji hao kuweza kupata asali nzuri
“Elimu ya
ufugaji nyuki kwa huku umasaini bado elimu hii haijasaamba ukilinganisha na
maeneo mengine”alisema Lyimo

No comments :

Post a Comment