Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa
warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Wadau wa sekta ya ujenzi
wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa (hayupo pichani), katika warsha ya sekta hiyo kuhusu uboreshaji
wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akizungumza jambo na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga
(kulia), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa
utendaji kazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Ujenzi (NCC), Prof. Mayunga Nkunya (kulia), akifafanua jambo na Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto),
jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la
Taifa la Ujenzi (NCC), Dkt. Samson Mturi akitoa taarifa kwa mgeni rasmi
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo
pichani), katika warsha ya wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu uboreshaji
wa utendaji kazi wa Baraza hilo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa
Mkurugenzi wa Huduma za Biashara Bw. Milton Lupa (aliyesimama), kutoka
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa
nyumba za magomeni, jijini Dar es Salaam.
Mkadiriaji Majenzi na Msanifu
Majengo Neema Kifua (wa pili kulia), akitoa taarifa kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo
ya mradi wa ujenzi wa nyumba za magomeni, alipotembelea mradi huo leo,
jijini Dar es Salaam.
………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya ujenzi
kuanza kuweka ...
twakwimu takwimu zinazohusu masuala ya ujenzi hapa nchini.
Akifungua warsha ya wadau wa sekta
ya ujenzi kuhusu uboreshaji wa utendaji kazi wa Baraza la Taifa la
Ujenzi (NCC), Prof. Mbarawa, amesisitiza umuhimu wa sekta hiyo
kuimarisha taarifa za aina, vifaa, viwango vinavyohitajika kimataifa na
gharama katika shughuli za ujenzi wa barabara, viwanja vya ndege, nyumba
na miundombinu mingine.
“Sekta ya Ujenzi ina mchango
mkubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi na kijamii hivyo uwepo
wa taarifa mbalimbali unahitajika ili kurahisisha uelewa wa wananchi wa
kawaida katika masuala ya ujenzi na gharama zake”, amesema Prof.
Mbarawa.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa
amewahakikishia wadau wa sekta ya ujenzi kuwa Serikali itaendelea kuweka
mazingira wezeshi ili kuhakikisha sekta hiyo inakidhi matarajio ya
watanzania wengi kwa lengo la kuwajengea miundombinu iliyo bora na
imara.
Ameongeza kuwa mapendekezo
yatakayotolewa na wadau hao yatarahisisha utekelezaji wa miundombiu
mbalimbali ambayo italeta chachu kwa sekta nyingine zikiwemo za kilimo,
nishati, utalii, viwanda, madini na uendelezaji wa biashara na nchi
nyingine za kikanda.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema ongezeko
la miradi ya ujenzi imechangia Serikali kutafuta wataaalm waliofanya
tafiti kwa ajili ya uboreshaji wa baraza hilo wataongeza tija na ufanisi
wa sekta hii muhimu ya ujenzi kwa wadau, wananchi na Serikali.
Naye, Mwenyekiti wa Baraza la NCC
Prof. Mayunga Nkunya amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa baraza lake litasimamia michango yote itakayotolewa na wadau hao na kuahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili NCC ikiwemo za takwimu ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua kwa kuwa ni sekta mtambuko.
Prof. Mayunga Nkunya amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa baraza lake litasimamia michango yote itakayotolewa na wadau hao na kuahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili NCC ikiwemo za takwimu ili kuhakikisha sekta hiyo inaendelea kukua kwa kuwa ni sekta mtambuko.
Sekta ya Ujenzi ni mojawapo ya
sekta zinazokua kwa kasi hapa nchini na ina mchango mkubwa kwa Pato la
Taifa ambapo mwaka 2016 sekta hiyo ilichangia asilimia 14 ya Pato la
Taifa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments :
Post a Comment