Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa
wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Khamis mara alipowasili katika
viwanja vya Sea Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B”
Unguja alipofanya ziara katika Wilaya hiyo leo,[Picha na Ikulu.] 12
/08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Haji Juma Haji mara
alipowasili katika viwanja vya Sea Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya
Kaskazini “B” Unguja alipofanya ziara katika Wilaya hiyo leo,[Picha na
Ikulu.] 12 /08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na
Makamanda wa vikosi vya ulinzi mara alipowasili katika viwanja vya Sea
Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja alipofanya
ziara katika Wilaya hiyo leo,[Picha na Ikulu.] 12 /08/2017.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai
Mwinyi Khamis na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serkali za
Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir (kushoto) pamoja na
Viongozi mbali mbali mara alipowasili katika Hotel ya Sea Cliff
Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja alipofanya ziara katika
Wilaya hiyo leo,[Picha na Ikulu.] 12 /08/2017.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali katika ukumbi wa mikutano wa
Hotel ya Sea Cliff Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja
katika Mkutano wa Ziara maalum ya kutembelea miradi mbali mbali ya
mendeleo kwa Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyoanza leo,kabla ya kupata
taarifa ya mkoa katika ukumbi huo,[Picha na Ikulu.] 12 /08/2017.
Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi CCM Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja na Viongozi wa Serikali ya
Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa utolewaji wa taarifa ya Mkoa wa
Kaskazini Unguja iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja
Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed (hayupo pichani) katika ukumbi wa Sea Cliff
Hotel Shehia ya Kama Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo,[Picha na
Ikulu.] 12 /08/2017.
Baadhi ya Washauri wa Rais na
Viongozi wengiine walipokuwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed (hayupo pichani) alipokuwa akitoa taarifa
yakee ya utelezaji wa majukumu ya Mkoa wa Kaskazi Unguja katika mkutano
uliofanyika leo katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Shehia ya Kama Wilaya
ya Kaskazini “B” Unguja mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,[Picha na
Ikulu.] 12 /08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein akibadilishana mawazo na Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Mohamed (kushoto) wakati
alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Tangi la Maji safi na Salama katika
Kijiji cha Kisongoni Upenja Wilaya Kaskazini “B” Unguja leo, akiwa
katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(wa pili
kulia) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud
Twalib,[Picha na Ikulu.] 12 /08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipokea taarifa ya
Utekelezaji Kazi ya Mkoa wa Kaskazini Unguja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo
Mhe.Vuai Mwinyi Mohamed baada ya kuisoma katika mkutano uliofanyika leo
katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Kama Wilaya ya Kaskazini “B”,Rais
alipofanya ziara maalum katika Wilaya hiyo kuangalia Miradi mbali mbali
ya Maendeleo,[Picha na Ikulu.] 12 /08/2017.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali
wa Chama na Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza
nao akiwa katika ziara ya kuangalia Miradi mbali mbali ya Maendeleo
katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Kama
Wilaya ya Kaskazini “B”,Unguja,[Picha na Ikulu.] 12 /08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na
Viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali (hawapo pichani) katika
mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel Kama Wilaya ya
Kaskazini “B”,Unguja,alipofanya ziara maalum ya kuangalia Miradi mbali
mbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo, [Picha na Ikulu.] 12 /08/2017.
…………………………………………………………………..
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMO Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka viongozi na watendaji wa
chama hicho kufanya kazi za kuimarisha taasisi hiyo ya kisiasa ili
ishinde na kuongoza dola katika uchaguzi mkuu ujao.
Rai hiyo ameitoa wakati
akizindua Tawi la CCM la Kitope ‘B’ jimbo la Mahonda kwenye ziara yake
ya kukagua na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo aliyoianza leo
Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Dkt. Shein alisema viongozi na
wanachama wa chama hicho wanatakiwa kutumia vyema ofisi za Tawi hilo
ambalo ni la kisasa kwa lengo la kutekeleza kwa ufanisi kazi za kisisaa
zitakazozaa matunda ya ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2020.
“Kwanza nakupongezeni viongozi na
wanachama wote wa jimbo la Mahonda mlioshiriki kujenga tawi hili la
kisasa linaloendana na hadhi ya chama chetu kimaendeleo kwani lina ofisi
zote ambazo ngazi zote kiutendaji ndani ya tawi mtafanya kazi zenu kwa
utulivu.
Pia nasaha zangu kwenu ni kwamba
uchaguzi mkuu unakaribia haupo mbali hivyo tumieni ofisi hii vizuri
kuchapa kazi kwa bidii sambamba na kuongeza wanachama wapya ambao ndio
mtaji wetu mkubwa wa kisiasa ili kuhakikisha 2020 tunashinda.”,
alisisitiza Dkt. Shein.
Aidha alisema kuwa lengo la
serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inayotokana na CCM ni kuimarisha
huduma zote za kijamii na kiuchumi ili wananchi wa mijini na vijijini
waweze kunufaika na fursa hizo.
Dkt.Shein ambaye pia ni Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alitembelea ujenzi wa
kituo kipya cha mashine za kutibia maji kinachojengwa katika eneo la
Donge mbiji ambapo mradi huo uliofadhiliwa na serikali ya China
utagharimu zaidi ya Dola za kimarekani milioni 5.5.
Katika ziara hiyo Dkt. Shein
alitembelea shamba la karafuu na kuzungumza na mliki wa mradi wa
kilimo cha karafuu huko Donge Pwani, Haroun Abou Mbarouk alieleza kuwa
shamba hilo lenye mikarafuu zaidi ya 170 limekuwa likizalisha zao hilo
kwa wingi ambapo kwa mavuno ya mwaka wanapata zaidi ya gunia 25.
Sambamba na hayo Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alitembelea mradi wa ujenzi wa
tangi la Maji huko Donge Kisongo unaojengwa na mafundi kutoka jamhuri
ya watu wa China utakaowanufaisha wananchi wa Wilaya ya Kaskazini “B”
na maeneo jirani.
Ziara hiyo itaendelea kesho
katika Wilaya ya Kaskazini ‘’A” Unguja ambapo Dkt.Shein ataweka mawe
ya msingi katika miradi mbali mbali ya kijamii na kuhitimisha kwa hotuba
ya majumuisho ndani ya Mkoa huo.
No comments :
Post a Comment