NAIBU
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema "
Wote scheme ni Mkombozi kwa wananchi wengi walio katika Sekta isiyo rasmi na
ameushahuri Mfuko wa Pensheni wa PPF kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii
kupitia Ofisi za Halmashauri ili kuweza kuwafikia kwa urahisi jamii ambayo
haipo kwenye ajira rasmi na kuweza kunufaika na Mfumo huo.
Mfuko
wa Pensheni wa PPF unashiriki katika
Maonesho ya Nane nane kitaifa Lindi kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa
wananchi hasa walio katika sekta isiyo rasmi kama vile
wakulima, wafugaji, Wavuvi, wajasiriamali wakubwa na wadogo na wengine wote
waliojiajiri wenyewe juu ya Mfumo wa " Wote scheme " ambao
unawawezesha kujiwekea akiba wakati huo huo wakipata fursa za mafao ya Uzeeni,
huduma za bima ya afya, mikopo ya maendeleo na mikopo ya kujiendeleza kielimu.
Vilevile
kwa wale walioajiriwa wanaweza kumtumia Mfumo huu wa "Wote
scheme" kama mfumo wa hiari wa kujiwekea akiba
Zaida
Mahava, Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya kusini amesema kwa kutambua
kundi kubwa la jamii ambalo halipo kwenye ajira rasmi wameona ipo haja ya kutoa
elimu juu Mfumo wa Wote scheme ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na
PPF kupitia Mfumo wa Wote scheme.
Naibu
Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (Mb) akiongea
jambo na Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava (kushoto) pamoja na
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF baada ya kupewa maelezo ya namna ya Mfumo wa
WOTE SCHEME unavyofanya kazi na faida zake kwa sekta isiyo rasmi wakati
alipotembelea Banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na
Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi
katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Meneja
wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava akimuelekeza Mwananchi jinsi ya kujaza
fomu ya kujiunga na mfumo wa hiari wa Wote scheme baada ya kupewa elimu
alipofika katika Banda la PPF lililopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango
katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya
Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (Mb) akusaini kitabu cha wageni
alipotembelea banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na
Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa
Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
No comments :
Post a Comment