Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven (kushoto aliyevaa miwani) akipokea
maelekezo kutoka katika moja ya mabanda ya SAGCOT.
NA
OFISI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA
MKUU
wa Mkoa wa Rukwa KamishnMstaafu Zelote Stephen ameishauri kamati ya maandalizi
ya nanenane nyanda za juu kusini kufikiria kushirikisha nchi za SADC ili
kuongeza hamasa na kuleta ushindani kwa watanzania wafahamu yanayofanyika
katika nchi za jirani.
Ametoa
ushauri alipokuwa akifanya majumuisho baada ya kutembelea mabanda 16 ya bidhaa
mbalimbali za kilimo katika maonesho ya nane nane kwa kanda ya nyanda za juu
kusini yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya ambapo Mh.
Zelote Stephen alikuwa mgeni rasmi wa siku ya tatu tangu ufunguzi wa maonesho
hayo.
“Tuachane
na mazoea, maonyesho haya yana miaka 25 sasa tuyaboreshe zaidi, isiswe ni mikoa
hii tu saba, tupanue wigo, kwakiwa huku ni nyanda za juu kusini basi tufikirie
kuzishirikisha nchi za SADC ambazo zitasaidia kubadilishana biashara na
teknolojia pamoja na kutafuta masoko,” Alifafanua.
Akisisitiza
suala hilo Mh. Zelote alibainisha kuwa nchi ya Tanzania inafikika kwa njia
zote, ardhini, majini na angani huku akitaja meli mbili zilizozinduliwa Mkoani
Mbeya na Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa, treni ya TAZARA pamoja na ndege
zinazomilikiwa na nchi yetu.
Aidha
amezishauri halmashauri kuanza maandalizi kwa kuwa na siku maalum kwaajili ya
maadhimisho hayo kihalmashauri ili kuwapa ujuzi na kujua ubora wa vitu ambavyo
vinaweza kupelekwa kwenye maadhimisho ya nanenane kikanda ili kuimarisha
ushindani na kumpa kila mwananchi nafasi ya kuelimika ili kuwa na kilimo chenye
tija.
Akiunga
Mkono Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sumbawanga Mh. Kilolo Ntila alityekuwemo katika msafara huo alisisitiza kuwa
maonesho ya nanenane yanayofanyika kikanda yanalenga watu wenye kipato cha
kutoka katika halmashauri zao na kukusanyika jijini Mbeya huku wakulima wasio
na uwezo wakikosa elimu inayopatikana kutokana na maonyesho hayo.
“Nikiongezea
aliyoyasema Mheshimiwa Mkuu wangu wa Mkoa, kwa nafasi yake namuomba aweze
kushawishi haya makampuni makubwa kuweza kusambaza wataalamu wao katika
Halmashauri zetu ambapo kuna uhitaji mkubwa wa elimu hii inayotolewa hapa
katika viwanja hivi vya nanenane na wao ndio walengwa wakubwa wa shughuli hii,”
alisema.
Pamoja
na hayo Mh. Zelote alitoa wito kwa wananchi wote wenye nafasi wajitokeze kwa
wingi kwenye maonyesho hayo ili waweze kuelimika kutokana na mafunzo mbalimbali
yanayotolewa viwanja hivyo vya nanenane na kusifu maandalizi ya sherehe hizo.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven (mwenye miwani) akiuliza kuhusu matumizi ya
mashine ya kukokota alipotembelea banda la Agricom
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven, akiangalia (buti), Kiatu cha kijeshi moja ya
bidhaa zinazotengenezwa na Jeshi la Magereza Mbeya
RC Rukwa
akijaribu kuendesha moja ya Trector za John Deere katika maonyesho ya Nanenae
Mbeya
RC Rukwa
akiwa ameshikilia "wheel chair" bidhaa inayotengenezwa na Jeshi la
magereza Mbeya
No comments :
Post a Comment