Waziri wa Habri, Sanaa na Michezo, Dkt.
Harrison Mwakyembe, akifurahia jambo kwa kupiga makofi wakati wa kikao
chake na wasanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava' kwenye ukumbi
wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam, leo Agosti 3, 2017. Wasanii wa muziki huo walieleza changamoto
mbalimbali zinazoukabili muziki wao na hivyo kushusha kipato chao ikiwa
ni pamoja na masuala ya mikataba mibovu pamoja na kuibwa kwa kazi za
wasanii
Dkt. Mwakyembe akipokea zawadi ya
mchoro wenye saa ya ukutani iliyotolewa na wasanii hao. Wanaokabidhi
zawadi hiyo ni Mwenyekiti wa wasanii hao wanaounda chama cha TUMA, Bw.
Brighton Mbwana, na msanii Witness Kibonge mwepesi.
Dkt. Mwakyembe akifurahia jambo na Naibu Waziri wake, Mhe.Anastazia Wambura
Hamorapa nae alikuwepo
Mwana FA, akifuatilia kwa makini kikao hicho.
Kaimu Katibu Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania, (BASATA), Bw. Onesmo Kayanda, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Bongho Flava, Bw.Brighton Mbwana akitoa hotuba yake.
Mwanasheria wa wamauziki Mwana FA na
AY, Bw.Albert Msando, akizungumza kwenye kikao hicho ambapo alieleza
udhaifu wa mikataba wanayoingia wasanii na makampuni unavyowatafuna.
Mhe. Dkt. Mwakyembe akimsikiliza kwa makini mwanasheria Msando
Mwanamuziki mkongwe nchini, Carola Kinasha, akizungumza
Baadhi ya wasanii walohudhuria kikao hicho
Msanii wa Bongo Flava, AY
Mhe. Dkt. Mwakyembe akiwasili kwenye ukumbi huo.
Wasanii wakongwe hawa wakiwa nimiongoni mwa walioshiriki mkutano huo.
Meza kuu.
AY akizungumza na mwanasheria wake, Albert Msando.
Witness akipeleka zawadi ya Mhe. Waziri.
No comments :
Post a Comment