Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi,George Simbachawene akifungua maonesho ya wakulima na wafugaji
Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akitembelea maonesho kwenye
vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed Co kabla ya kufungua maonesho ya
wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya
Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa
kampuni hiyo,Philemon Mushi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akitembelea maonesho kwenye
vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed Co kabla ya kufungua maonesho ya
wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya
Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa
kampuni hiyo,Philemon Mushi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(kulia)akipewa
maelezo ya namna ya kulima bila kutumia udongo na Mtalaamu wa kilimo wa
kampuni ya Rijk Zwaan alipotembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni
ya mbegu hiyo kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akiangalia namna kikundi
cha Nronga Women Dairy cha wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro
kinavyojishughulisha na uuzaji wa maziwa kwenye banda la halmashauri ya
Hai kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa
Hai,Gelasius Byakanwa.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza kwenye maoenesho ya 24 ya wakulima na wafugaji kanda ya kaskazini .
……………………………
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Nane nane ni miongoni mwa
maonyesho maarufu Nchini Tanzania ambayo huwagusa na kuwakutanisha
wakulima, wafugaji, wavuvi wa Mjini na Vijijini, Taasisi za Serikali na
binafsi zinahusika na sekta hiyo zilizopo ndani na nje ya Nchi pamoja na
Wadau wa Kilimo.
Maonyesho ya Nane nane hutoa fursa
kwa wadau wote wa sekta ya ...
Kilimo kuonyesha bidhaa mbalimbali za
Kilimo, kuuza bidhaa hizo, kubadilishana uzoefu na kujifunza teknolojia
mbalimbali zia kuboresha Sekta ya Kilimo ili kuondokana na Kilimo cha
kufa na kupona na kuwa Kilimo chenye Tija kinanachofaa kwa biashara na
kutosheleza kwa chakula.
Katika historia ya maonyesho haya
ambayo wakulima kutoka Halmashauri mbalimbali Nchini hushiriki ili
kujifunza teknolojia hizo mpya za Kilimo kumekuwa na mabadiliko kidogo
katika eneo la utekelezaji wa Teknolojia hizo katika maeneo yao.
Huenda tatizo likawa ni uelewa
mdogo wa wakulima wetu wanaoshiriki katika maonyesho hayo, kutokujifunza
kwa umakini kuhusu mbinu hizo za kisasa au kukosekana kwa uwezeshaji
wa wananchi katika kutekeleza mbinu hizo kwenye maeneo yao au kutokuwa
na usimamiza wa maafisa Ugani katika maeneo mengi ya Kilimo Nchini.
Ushiriki wa mazoea katika
Maonyesho haya unaelekea kufika mwisho baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene
kufungua Maonyesho ya 24 Kanda ya Kaskazini yaliyofanyiika Mkoani Arusha
katika viwanja wa Themi – Njiro.
Wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho
hayo Waziri Simbachawene alikagua mabanda mbalimbali ya Kili mo na
Mifugo ya Halmashauri za Kanda ya Kaskazini, Sekta binafsi za Kuzalisha
Mbegu bora, Pembejeo, Zana za Kilimo viwatilifu pamoja na dawa za Mifugo
na kujionea teknolojia bora na za kisasa zinazoweza kumsaidia Mkulima
na Mfugaji kuachana na kilimo cha kujitaftia chakula na kuhamia kwenye
biashara njia itakayoweza kumuo ngezea kipato na kumwinua kiuchumi.
Akifungua Maonyesho hayo Mhe.
Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauro zote Nchini sambamba
na Maafisa Ugani kujifunza Teknolojia mbalimbali zilizopo kwenye
maonyesho haya na kwenda kuwafundisha wananchi na kuwawezesha
kuzitekeleza katika maeneo hayo.
Amesema kuanzia mwaka huu nataka
maonyesho haya yanalete mabadiliko kwa wananchi wetu kwa kuwawezesha
kulima kwa Tija kwa kutumia eneo dogo na kuweza kupata mazao mengi,
kufunga kisasa kwa kuwa na mifugo bora na michache lakini yenye faida
kubwa pamoja na kuanzisha ufugaji bora wa samaki katika maeneo mengi
Nchini.
“Kuanzia mwakani tutaanza kufanya
tathmini ya namna ambavyo maonyesho haya yamebadilisha maisha ya
wakulima wetu katika Halmashauri na sio kila mwaka Halmashauri
zinashiriki lakini hamuondoki na kitu kipya wala hamuwasaidii wakulima
wa kule vijijini ambao huenda hawapati fursa ya kuja kuona mapinduzi
haya katika Kilimo”.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya maonyesho haya Kanda ya Kaskazini amesema katika mara
hii ya kwanza ambapo maonyesho haya yametoka kwenye Chama cha Wakulima
na Wafugaji (TASO) na kuratibiwa na Serikali wamejitahidi kushirikisha
wadau mbalimbali wenye teknolojia tofauti tofauti ili kuweza kutoa wigo
mpana kwa wakulima na wafugaji kujifunza zaidi.
Pia aliongeza kuwa ameunda kamati
ambayo itaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro
kuchunguza namna ambavyo TASO walivyokuwa wanafanya kazi, Mali
zinazomilikiwa na Taso, Mapato yaliyopatikana wakati wa uratibu wao na
namna ambavyo yalitumika na mgawanyo wa kazi zao na kuja na usahuri wa
kitaalam juu ya nini kifanyike katika kuboresha zaidi usimamizi wa
maonyesho hayo.
Waziri Simbachawene amefungua
maonyesho haya ikiwa ni ya Pili tangu maadhimisho ya Sherehe hizi
yalipoanza na alifungua Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo – Lindi na
atafunga maoneysho katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.
No comments :
Post a Comment