Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na baadhi ya
Viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akipoka bendera ya Taifa toka
kwa Wanariadha Aphonce Simbu na wenzake baada ya kuwasili toka nchini
Uingereza kwenye Mashindano ya Marathon ya 2017.
Mwanariadha Alphonce Simbu
akiwashukuru Viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea na kumpongeza kwa
ushindi wake katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017
ambapo aliweza kujinyakulia medali ya shaba.
Wazazi wa Mwanariadha Alphonce
Simbu wakiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba
aliyoshinda mtoto wao katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa
mwaka 2017.
Mwanariadha Alphonce Simbu
akiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba
aliyoshinda katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017.
Simbu akipokelewa na mashabiki wake akiwa amembeba mtoto wake
Simbu alifanikiwa kumaliza katika
nafasi ya tatu nyuma ya Tamirat Tola (Ethiopia) aliyemaliza nafasi ya
pili na Geoffrey Kirui (Kenya) aliyeibuka mshindi wa mashindano hayo kwa
upande wa wanaume.
Waziri Mwakyembe amewapongeza wanariadha wote waliokwenda London kuiwakilisha Tanzania na kufanikiwa kurudi na medali.
………………..
MSHINDI wa tatu wa Mbio za Dunia
za London Marathon mwaka huu, Felix Simbu amesema kuwa ushindi huo
alioupata si wapeke yake bali wa wanariadha wote ambao walienda
kushiriki kutokana walijitoa muhanga hadi kufanya vizuri.
Simbu alishika nafasi ya tatu
katika mbio za Km 42 na kuitoa kimasomaso Tanzania ambayo ...ilikuwa
haijafanya vizuri katika mashindano hayo kwa miaka mingi.
Akizingumza na Mtandao huu wa
www.Fullshangweblog.com, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa akitokea nchini Uingereza na kupokelewa na mamia ya mashabiki,
Simbu alisema haikuwa kazi rahisi kupata medali hiyo imetokana na wao
kujitoa muhanga.
“Ushindi huu si wangu peke yangu
bali ni wa wetu sote kutokana tulikuwa na umoja.”Huu ni ushindi wa
wote, hivyo umoja wetu utazidi kujitahidi kufanya vizuri zaidi hapo
baadae,” alisema.
Alisema, aliona kama maajabu kwa
ushindi huo baada ya kuona bendera ya Tanzania inapandishwa kuashiria
ushindi wake.Awali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Harryson Mwakyembe alisema ushindi huo umewafanya Watanzania wawe na
furaha kutokana hawakuwa na imani ya kufanya vizuri.
Alisema ni wakati sasa wa
kuwekeza katika mchezo huo ili uweze kupiga hatua zaidi. Simbu
aliwasilia saa 12:20 jioni kutokana na kuchelewa kufika ambapo awali
aliyatarajiwa kufika saa 6:05 mchana.
Kufika kwake alipokelewa na vikundi mbalimbali vya ngoma, wasanii ambao waliongozwa Khadija Kopa na Riyama Ally.
No comments :
Post a Comment