Baadhi
ya madiwani wa Baraza hilo,wakifuatilia taarifa ya mwanasheria wa
halmashauri juu ya madai ambayo wanahudai mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM)
Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo,Leornad Kiganga Bugomola,akielezea msimamo wa baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo juu ya madai ya mgodi. |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly akijibu baadhi ya maswali. |
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini.Constatine Kanyasu akichangia ajenda ya swala la malipo ya mgodi kwa halmashauri hiyo. |
Mwakilishi wa mgodi wa GGM Kwenye baraza Hilo Bw Joseph Mangilima akitoa ufafanuzi juu ya madai ambayo yanadaiwa na Halmashauri. |
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Halmashauri ya mji wa Geita imeitaka kampuni ya madini ya dhahabu ya Geita (GGM) kulipa kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya milioni 11.045 ambazo ni madai ukwepaji wa kodi ya huduma kwa kipindi cha mwaka 2004 hadi 2013 nakuipa muda wa mwezi mmoja endapo ...itashindwa itaupeleka Mgodi Mahakamani.
Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita Eng. Modest
Apolinary,Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu,Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Constantine Morandi na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola.
Mgodi
wa GGM ulianza uzalishaji mwaka 2000 na kuingia makubaliano na Wizara
ya nishati na madini ya kulipa dola 200,000 kwa halmashauri kila mwaka
lakini inadaiwa haikulipa hadi mwaka 2004 kwa madai kuwa halmashauri
haina sheria inayoelekeza walipwe kiasi hicho.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola amesema kuwa wametoa
siku 30 fedha zilipwe na endapo hawatalipwa basi wataupeleka mgodi
Mahakamani kwakuwa sheria zipo wazi inayowataka kulipa asilimia 0.03
Awali
akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Mwanasheria wa
Halmashauri ya mji Queen Luvanda amesema Madai hayo yanatokana na kodi
ya huduma ambayo kampuni ilipaswa kulipa kwa mujibu wa sheria.
Mwaka
2004 Halmashauri ilitunga Sheria ndogo ya kodi ya huduma ya asilimia
0.03 ya mauzo ya mwaka na kuanzia sheria itungwe mgodi hawakulipa
asilimia 0.03 bali walilipa dola laki mbili kuanzia mwaka 2004 hadi 2013
kinyume na maelekezo ya sheria inavyosema.
Maneja
Kitengo cha Mahusiano katika Mgodi wa GGM Joseph Mangilima amesema
sheria ya kodi ya huduma ilitungwa mwaka 2004 na ikaanza kufanya kazi
mwaka 2005 na Kampuni ilikua ikilipa dola 200,000 kila mwaka kwa mujibu
wa sheria
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
No comments :
Post a Comment