Baadhi ya wadau wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo wakati alipokuwa akizungumza.
NA JOEL MADUKA WA MADUKA ONLINE
Mgodi wa
dhahabu wa Acacia Bulyanhulu ambao upo kwenye Halmashauri ya Msalala Wilaya ya
Kahama Mkoani Shinyanga ,umekabidhi hundi ya yenye thamani ya shilingi milioni
mia mbili na ishirini na sita,laki Tisa ishirini na nane Elfu na mia moja kumi
na tano na senti sabini na sita(226,928,115,76) kwa ajili ya ushuru wa huduma
kwa halmashauri ya Nyang’hwale.
Kiasi hicho
cha fedha ni asilimia 33% ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipinidi
cha miezi sita yaani Januari hadi mwezi Juni mwaka Huu ,kiasi ambacho ni
asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma kwa mgodi huo kwa kipindi
husika.
Akikabidhi
hundi hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi Huo
,Graham
Crew,amesema kuwa jumla ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha
miezi sita iliyopita ni shilingi za Kitanzania ,Milioni mia sita ,themanini na
saba,laki sita na sitini elfu ,mia tisa hamsini na sita na senti themanini na
nne (687,660,956,84) na kwamba malipo hayo yamegawanywa kwenye halmashauri
mbili Kwa Mujibu wa makubaliano na serikali
ambapo Halmashauri ya Msalala imepata asilimia 67% na Nyang’hwale 33% hivyo katika kiasi hicho ,halmashauri ya
Msalala imelipwa kiasi cha Shilingi Milioni mia nne sitini,laki saba thelathini na mbili Elfu mia
nane arobaini na moja na sent inane(460,732,841.08) .
Aidha kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Carlos Gwamagobe,amesema kuwa fedha ambazo zimekuwa
zikitolewa zinasaidia katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa ni
pamoja na kujenga madarasa na kukarabati majengo ambayo ni chakavu.
Mkuu wa
Wilaya Hiyo,Hamim Gwiyamba ,amekili kuwepo kwa athari kutokana na mapato
kupungua kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye mgodi wa acacia na kwamba kuna huduma
za maendeleo zinaweza kupunguzwa kutokana na kupungua kwa Fedha.
Hadi sasa
mgodi huo umelipa zaidi ya Shilingi Bilioni 10,200,000,000 tangu mwaka 2000 kama
kodi ya ushuru wa huduma.Kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa
huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika mwaka 2014,kutoka kiasi cha Dola
200,000 kwa mwaka iliyokuwa inalipwa kama kodi ya ushuru wa huduma ya miaka ya
nyuma.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.
|
No comments :
Post a Comment