Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Makame Mnyaa Mbarawa(katikati), akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Bw. Le
Van Dai (kulia) wakati wakisaini mkataba wa kusambaza mawasiliano ya
simu kwa
kujenga miundombinu maeneo ya vijijini, chini ya Mradi wa sita wa
kufikisha
mawasiliano kwa wote, kwenye makao makuu ya UCSAF barabara ya Bagamoyo,
Kijitonyama jijini Dar es Salaam Agosti 18, 2017. UCSAF imesaini
makubaliano kama
hayo na makampuni mengine ya simu hapa nchini ikiwemo, Vodacom Tanzania
PLC,
Airtel, tigo na TTCL.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Mawasiliano Kwa Wote Nchini,
(UCSAF), umesaini mkataba na makampuni matano ya simu hapa nchini wa
utekelezaji wa Mradi wa Sita wa Kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote.
Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Manyaa Mbarawa.
Makampuni yaliyotia saini mkataba huo
ambao utayawezesha, kujenga miundombinu ya kupeperusha mawasiliano ya
simu kwenye mmbalimbali hususan vijijini ni pamoja na Halotel, Airtel,
Vodacom Tanzania PLC, TTCL na TIGO.
Waziri Profesa Mbarawa alishuhudia
Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF kwa niaba ya Mfuko, akisaini mikataba hiyo
na Maafisa Watendaji Wakuu wa makampuni hayo mbele ya waandishi wa
habari.
Kwa
mujibu wa maafisa wa UCASAF, kusainiwa kwa mikataba hiyo ni moja ya kutekekeleza
malengo makuu ya Mfuko ambayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya
mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano
hafifu.
Lakini
pia ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa
huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini yenye mawasiliano
hafifu.
Malengo mengine ni pamoja na Kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo
ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
Kutengeneza
mfumo kwa ajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi na
zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji katika soko la kiushindani;
Maafisa
hao wamesema lengo linguine ni kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango
nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasilianpo inapatikana
vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa, amewahakikishia wawekezaji ushirikiano uklio dhahiri kutoka serikalini
na kuwataka, waongeze kasi ya uboreshaji wa mawasliano ya simu ili wananchi
hususan wa vijijiniwaweze kutumia teknolojia ya mawasiliano kuharakisha
maendeleo yao.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa, akitoa hotuba yake
Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Bw. Joseph Kilongola, akizungumza kwabla ya kumkaribisha Profesa Mbarawa kutoa hotuba
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, akielezea lengo
la kusainiwa kwa mikataba hiyo ya utekelezaji wa Mradiwa sita wa
kupeleka mawasiliano kwa wote.
Baadhi ya wawakilishi wa makampuni ya simu
Bi. Beatrice Singano Malya kutoka Airtel, akifurahia hotuba.
Baadhi ya maafisa wa makampuni ya simu na UCSAF
Afisa kutoka kampuni ya Halotel
Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter
Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice
Suingano Malya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa
kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa,
(kulia), akimpongeza Mwakilsh wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi.
Beatrice Singano Malya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa
Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote, (UCAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017
Afisa
Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter
Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice
Singano Malya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa
wote.
Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Ian Ferrao, wakibadilishana hati baada ya
kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini.
Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, wakisaini mkataba huo
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, wakibadilishana hati baada ya
kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini.
UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini kwenye hafla
iliyofanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa
Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Mhandisi Cecil Nkomola Francis, wakisaini mkataba huo
Mhandisi Ulanga, akimpongeza Bw. Ferrao wa Vodacom
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, akiwa miongoni mwa maafisa wenzake wakisikiliza hotuba ya Mhe. Waziri
Profesa Mbarawa, akipena mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Bw.Joseph Kilongola.
Wakuu wa makampuni ya simu za mikononi nchini.
Bw. Ferrao, akitoa hotuba ya shukrani kwa niaba ya wenzake
Profesa Mbarawa na Mhandisi Ulanga, wakionyeshana kitu
Profesa Mbarawa akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Bw.Joseph Kilongola,
Baadhi ya maafisa wa makampuni ya simu na UCSAF
No comments :
Post a Comment