Friday, August 4, 2017

MAMLAKA ZA TANZANIA NA KENYA ZAKUTANA MPAKANI NAMANGA WILAYANI LONGIDO KUZUNGUMZIA VIKWAZO VYA KIBIASHARA

Viongozi na watendaji wakuu wa serikali na taasisi zake kutoka nchi za Kenya na Tanzania wakiwa Namanga wilayani Longido kwa majadiliano juu ya vikwazo vya bidhaa kadhaa vilivyoibuka hivi karibuni katika mpaka huo. Timu za nchi hizo mbili zimeongozwa na Makatibu Wakuu wa Biashara Prof. Adolf Mkenda kutoka Tanzania na Dr. Criss Kiptoo kutoka Kenya. Pichani walioketi mbele ya laptop ni Makatibu Wakuu huku wakiwa wamezungukwa na wataalam wa nchi zote mbili. Mbele yao kushoto ni Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kicheere na DC Longido Daniel Chongolo. Makatibu Wakuu hao walikuwa wakiandaa tamko la pamoja baada ya majadiliano yaliyodumu kwa saa 9 juu ya vikwazo kwa bidhaa kadhaa za Tanzania kwenda Kenya ukiwemo Unga wa ngano na LPG Gas.

No comments :

Post a Comment