Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimkabidhi zawadi Balozi wa
Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kushoto), baada ya mazungumzo na Balozi
huyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jjini Dar es Salaam leo.
Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi
kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga
mbalimbali. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na Balozi wa Kuwait
nchini, Jasem Al-Najem (Wakwanza kulia) alipotembelea Makao Makuu ya
Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo
aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika
masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali. Wengine ni Maafisa
Waandamizi wa Jeshi hilo.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem
Al-Najem, akizungumza wakati wa kikao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (katikati) na Maafisa Waandamizi
wa Jeshi hilo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam
leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo
kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga
mbalimbali.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiongozana na Balozi wa
Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kulia) alipowasili Makao Makuu ya Jeshi
hilo jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano
kati ya Majeshi ya nchi hizo kubadilishana Utaalamu katika masuala ya
kukabiliana na majanga mbalimbali.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem
Al-Najem, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati
alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa
mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye(hayupo
pichani). Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi
hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga
mbalimbali.na Uokoaji
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiwa katika picha ya pamoja
na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (katikati) baada ya kikao
cha mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi hizo
katika kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga
mbalimbali.
……………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Nchini, liko katika mkakati wa kuingia ushirikiano na Serikali ya Kuwait
katika shughuli zake za kukabiliana na majanga ya moto ikiwa ni juhudi
zake katika kuyafikia maeneo mengi nchini.
Akizungumza alipotembelea Makao
Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es salaam, Balozi wa
Kuwait Nchini, Jasem Al-Najem, alisema serikali ya Kuwait ipo tayari
kubadilishana mafunzo na kutoa msaada wa vifaa kwa Jeshi hilo.
“Ni vema tukatengeneza mpango
ambao wataalam wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka nchini Tanzania
wataweza kubadilishana uzoefu na wataalamu kutoka nchini Kuwait kwa
ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na majanga pindi
yanapotokea, ’’ Alisema Balozi huyo.
Akizungumza wakati wa kikao
hicho, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias
Andengenye alimshukuru kwa kumtembelea na kusema kuwa ujio wa balozi
huyo, umefungua ukurasa mpya kwa upande wa misaada na mafunzo kwa Askari
wa Jeshi hilo, kwani watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza
tija kwa Jeshi lake.
“Tutapata nafasi ya kubadilishana
uzoefu na kupata mafunzo kutoka Nchi ya Kuwait na kuongeza ufanisi
katika majukumu yetu ya kila siku, lengo ikiwa ni kukabiliana na majanga
mbalimbali yakiwemo ya moto,’’ alisema Kamishna Jenerali.
Katika kikao hicho Balozi wa
Kuwait, Nasem Al-Najem alipokea taarifa ya changamoto zinazolikabili
jeshi hilo ikiwemo uhaba wa vitendea kazi huku akiahidi kuzifanyia kazi
na akisisitiza mchakato wa kusaini makubaliano ya hiari ukamilike kwani
utakuwa msaada wa kutekeleza kwa haraka program za mafunzo ya muda
mfupi.
No comments :
Post a Comment