Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea eneo la mapokezi la hospitali ya
Tarime na kuagiza lijengwe banda kwa ajili ya kukaa wananchi badala ya
kukaa juani kama ilivyo hivi sasa.
Watumishi wa Halmashauri mbili za Tarime wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Majengo yaliyojengwa na wadau wa mgodi wa North Mara kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Tarime.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime.
……………………………………………………………….
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
Tamisemi Selemani Jafo amewataka watumishi wa halmashauri ya mji wa
Tarime na Halmashauri ya wilaya ya Tarime kuacha tabia ya...kufanyakazi
kwa mazoea.
Jafo aliyasema hayo alipokuwa
akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri hizo mbili wakati wa ziara
yake leo wilayani Tarime mkoani Mara.
Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kutembelea miradi ya afya, elimu, daraja na ujenzi wa nyumba za watumishi.
Jafo ameiagiza viongozi wa
halmashauri hizo mbili kukaa na kufanya maamuzi ya majengo ya
halmashauri ya wilaya ya Tarime yaliyopo ndani ya eneo la halmashauri ya
mji yatumike kwa matumizi ya kiofisi ya halmashauri ya mji.
Aidha ameagiza fedha
zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa halmashauri ya mji zihamishiwe
halmashauri ya wilaya ili waende kuanza ujenzi wa ofisini katika eneo
lao badala ya kukaa ndani ya eneo la halmashauri mji.
“Kitendo hichi kinawakosesha
wananchi haki yao ya kupata huduma kwa ukaribu jambo ambalo ndilo
lilikuwa msingi wa kugawa halmashauri hizo,”amesema Jafo
Naibu Waziri Jafo amemaliza ziara yake na kuelekea wilaya ya Rorya, mkoani Mara.
No comments :
Post a Comment