
NA VERONICA KAZIMOTO
WADADISI wa Utafiti wa
Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 wameaswa
kuzingatia maadili ya kazi wakati wa zoezi la kuorozesha kaya linalotarajia
kuanza kesho ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utafiti huo.
Akizungumza wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika jijini
Dar es Salaam kwa wadadisi hao, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema ili kufanikisha zoezi la uorodheshaji
wa kaya, ni lazima wadadisi hao wakazingatia maadili ya kazi pamoja na kufuata
taratibu zote za Utumishi wa Umma.
“Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawaagiza kwenda kwenye jamii kwa
ajili ya kuorodhesha kaya zitakazofanyiwa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Natumaini mtatii na kuheshimu maadili
ya Utumishi wa Umma ili muweze kufanikisha kazi hii kwa ufanisi,” amesema
Slyvia Meku.
Amesema Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya litafanyika mikoa yote ya
Tanzania Bara kwa takribani siku 15 kuanzia kesho Julai 11, 2017 na baadae
kufuatiwa na utafiti wenyewe unaotarajia kuanza mwezi Desemba, 2017.
Sylvia Meku amesema utafiti huu unafanywa na Ofisi
ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya
Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuangalia kiwango cha umasikini nchini.
Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia
Meku akizungumza wakati wa mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya
mikoa yote kwa ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya
litafanyika kwa muda wa siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai,
2017.
Baadhi ya Wadadisi wakimsikiliza kwa makini
Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu Bi. Sylvia Meku (hayupo Pichani) wakati wa
mafunzo ya Wadadisi watakaokwenda kuorozesha kaya mikoa yote kwa ajili ya
maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa
Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa siku kumi
na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.
Baadhi ya Wadadisi wakielekezwa namna ya
kutumia ramani wakati wa kufanya mazoezi ya kuorozesha kaya kwa vitendo na
Mtalaam wa Ramani Jumanne Msuya wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (katikati) kwa
ajili ya maandalizi ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania
Bara wa Mwaka 2017/18. Zoezi hilo la uorozeshaji kaya litafanyika kwa muda wa
siku kumi na tano (15) kuanzia kesho tarehe 11 Julai, 2017.(PICHA ZOTE NA
EMMANUEL GHULA)



No comments :
Post a Comment