Waziri
Ummy akimjulia hali akina mama waliojifungua katika wodi ya
Wazazi.Akina mama hao walikiri kuhudumiwa vizuri na watoa huduma hiyo
pia hawajatozwa fedha yeyote kama sera ya afya inayosema kila mama
mjamzito matibabu ni bure
Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu akiongea
na watoa huduma kwenye hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Geita wakati
alipofanya ziara ya kikazi katika hospitali hiyo ambapo aliridhishwa na
huduma zitolewazo na hospitali hiyo na kuwapongeza kwa kuanzisha
kitengo cha ubora za huduma za faya ambacho kinasaidia kuimarisha afya
ya wagonjwa ikiwemo mama na mtoto pamoja na lishe.Kushoto ni Mkuu wa
Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga na nyuma ya Waziri ni
Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita Thomas Dimme
Mhudumu
wa afya pekee wa kike katika chumba cha kuhifadhi maiti Bi.Angela
Milinga(mwenye koti jeupe) ambaye anafanya kazi katika hospitali hiyo
akimshukuru Waziri Ummy kwa kufika katika kitengo chake na kujionea
jinsi wanavyofanya kazi .
Mhudumu
wa chumba cha kuhifadhia maiti Bi. Anjela akieleza jinsi anavyofanya
kazi kwa Mhe. Waziri (hayupo pichani) mara baada ya kutembelewa na ugeni
huo.
Watumishi
wa hospitali hiyo wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa ndani
mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za kutolea huduma za
hospitali hiyo
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Dkt. Joseph Kisala akisoma taarifa ya hospitali
hiyo,Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mhe.Costantine Kanyasu na
Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Brian Mawalla
Mganga
Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Brian Mawalla akimfafanulia jambo
Waziri wa afya(hayupo pichani) wakati wa mkutano na watumishi wa
hospitali hiyo
Picha
ya Pamoja ya Waziri Ummy Mwalimu, Viongozi wa Mkoa,Wilaya na watumishi
wa hospitali hiyo mara baada ya kumaliza mkutano wa ndani.Katika kikao
hicho Waziri aliwataka wafanyakazi ambao hawataki kubadilika na
kuwajibika wakati wa kuwahudumia wagonjwa wapishe kwani hivi sasa kuna
wahitimu wengi wanahitaji ajira Serikalini hususan kada ya afya.(Picha zote na Wizara ya Afya)
No comments :
Post a Comment