Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe
akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style,
lililofanyika makumbusho ya Taifa Jijini Dar ,linalohusisha fani za
ubunifu wa mavazi,upigaji picha na uandishi wa miswada ya filamu ambapo
aliipongeza Taasisi isiyo ya kiserikali ya Faru Arts and Development
Organization(FASDO) kwa kuandaa mashindano hayo, alisema kuwa Serikali
inalojukumu la kusaidia Asasi kama FASDO ambazo zinaingia katika maswala
ambayo Serikali hawakuyawekea msingi mkubwa. "Naomba niagize na kuwa
kuna watendaji wetu wa wizara katika sherehe hii mkae chini na watu wa
FASDO ili mwaka kesho zoezi hili lifanyikie Bungeni Dodoma" Alisema Dkt.
Mwakyembe.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa
tatu kutoka kulia) akimkabidhi Agnes Nyahonga tuzo na zawadi ya mfano
wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda shindano la Bongo
Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili
kutoka kulia) akimkabidhi Goodhope Elieskia maarufu kwa jina la Zagamba tuzo na zawadi ya mfano wa
Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda shindano la Bongo
Style katika kipengele cha uandishi wa miswada ya Filamu
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh. Dkt. Harrison Mwakyembe(wa
kutoka kulia) akimkabidhi Masoud Masoud tuzo na zawadi ya mfano wa
Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda shindano la Bongo
Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh. Dkt. Harrison Mwakyembe(wa
pili
kutoka kulia) akimkabidhi Philip Florian tuzo ya Best Personality
aliyopokea kwa niaba ya Kelvin Mwanasoko ambaye hakuweza fika katika
Mashindano hayo.
Msanii Dullah Aka DY akitumbuiza wakati wa Fainali hizo
Katibu
Mkuu wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza
wakati wa fainali za Shindano la Bongo Style na kuipongeza Asasi ya
Kiraia ya FASDO kwa ubunifu mkubwa.
Mratibu
wa FASDO Nchini Tanzania Bi. Joyce Msigwa akizungumza wakati mambo
mbalimbali yanayohusu Asasi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio
waliyoyapata kama kuendesha shindano la Na mimi nipo pamoja na FASDO CUP
na mengine mengi yahusuyo asasi hiyo.
Ilikuwa
ni 'Surprise' Kati kati ya Sherehe za Shindano la Bongo Style ambapo
Mratibu Mkuu wa FASDO na Muasisi wa Asasi hiyo isiyo ya kiserikali Bi.
Lilian Nabora(Aliyevaa Gauni Jekundu) alipofanyiwa Hafra fupi ya siku
yake ya Kuzaliwa ambapo alitimiza miaka 50. Waliomsindikiza ni 'Team' ya
FASDO pamoja na washiriki wa shindano hilo kwa mwaka 2017.
Mratibu
Mkuu na Muasisi wa FASDO Lilian Nabora akiongea wakati wa fainali za
Bongo Style, alisema kuwa wamewekeza sana katika mitandao ya kijamii na
hasa tovuti ya www.fasdo.org ili
kuwafikia vijana wengi zaidi Tanzania nzima ambao wanauwezo na
wanajiamini kuwa wanavipaji katika mambo mbalimbali wapate kujiunga
katika taasisi hiyo,aliongeza kuwa mchakato wa kuwapata washindi
ulipitia mchujo mpaka kuwapata washiriki bora 30,kisha 15, mpaka kufikia
washindi watatu(3) "Mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana wanaokadiliwa
kuwa 1,500 na mpaka sasa bado tunawahimiza wapate kujiunga nasi" alisema
Bi. Lilian.
Waliokaa
katika Meza ni Majaji Upande wa ubunifu wa mavazi, na walio mstari wa
mbele ni Majaji upande wa Miswada ya Filamu na upigaji picha.
Baadhi ya washiriki upande wa Ubunifu wa Mavazi wakiwa wanaonesha Mavazi yao waliyo yabuni wao wenyewe
Wageni waalikwa wakifuatilia sherehe za Fainali za shindano la Bongo Style
Mwenyekiti wa FASDO Bw. Stanley Kamana akitoa neno la Shukurani wakati wa Fainali za Bongo Style
Washiriki wa Shindano la Bongo Style kwa Mwaka 2017 wakiwa wanafuatilia mambo mbali mbali wakati wa Shindano hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Asasi ya Kiraia ya FASDO Bw. Tedvan Nabora akitoa neno la
Shukurani kwa wote waliohudhuria katika Fainali za shindano la Bongo
Style
Picha ya pamoja ya Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison
Mwakyembe,Uongozi na Team ya FASDO,Majaji na washindi wa Bongo Style
Competition kwa mwaka 2017. (Picha zote na Laden Tedvan Nabora).
No comments :
Post a Comment