Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
Serikali imesema kuwa jumla ya vijiji 7873 na vitongoji vyake vyote hapa nchini vitakuwa vimeshaunganisha na umeme chini ya Mradi wa Umeme Vijijini Awamu wa Tatu ifikapo... mwaka 2021.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri.
Dkt.
Kalemani alisema REA III itasaidia kukamilisha vijiji vilivyobaki
ambavyo havijaunganishwa na umeme ifikapo mwaka 2021 kwa ajili ya
kuchochea maendeleo ya uchumi kati kuelekea uchumi wa viwanda.
Alisema
kuwa lengo la Serikali ni kutaka wananchi wote hata wale wanaoishi
visiwani waweze kufikiwa na huduma ya umeme kwa ajili ya matumizi yao na
kwa ajili ya uendeshaji wa viwanda.
Aidha
kwa upande wa Mkoa wa Tabora alisema vijiji vipatavyo 510 na vitongoji
vyake vinatarajiwa kuwa vimeshaunganishwa na umeme wa uhakika wa ifikapo
mwaka 2021 kupitia mradi wa REA III.
Aliongeza
kuwa ili kuhakikisha lengo hilo la kuunganisha vijiji vyote vinakuwa na
umeme, Serikali imeamua kuweka Wakandarasi wengi katika kila mradi na
kuwaagiza kugawa kazi kwa Wakandarasi wadogo ambao ni wazawa na wenye
sifa ili kurahisisha kazi na kuifanya iwe na ufanisi.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alisema kukamilika
kwa mradi wa REA III utaufanya mkoa huo kukua kwa kasi zaidi na kutoa
wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika viwanda vya sekta mbalimbali
ikiwemo za usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo na uchimbaji madini.
Alisema kuwa hivi sasa Mkoa huo unazidi kuimarika katika miundombinu ya barabara , reli , anga na upatikanaji wa maji na umeme wa uhakika na hivyo kutokuwepo na vikwazo katika uzalishaji.
Uzinduzi
wa uunganishwaji mradi wa umeme vijijini kwa awamu ya tatu unatarajiwa
kufanyika tarehe 1 Agosti 2017 katika Wilaya ya Sikonge kwa niaba ya
Wilaya zote za Mkoa wa Tabora.
No comments :
Post a Comment