Mtangazaji wa Televisheni ya
Everton, Darren Griffiths, akizungumza na wagonjwa waliotibiwa na
kufanyiwa upasuaji wa Mabusha na Matende nchini Tanzania wakati
walipokutana katika hoteli ya Seacliff jijini Dar es Saalam Timu hiyo
ipo nchini kwa mchezo mmoja wa kati yao na timu ya Gor Mahia ya Kenya
ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza inayotarajiwa
kuanza mwezi ujao.
Timu ya Everton imekuwa
ikifadhili matibabu ya wagonjwa wa Mabusha na Matende kupitia Taasisi ya
LSTM Surppoting Tanzania Program ya Liverpool nchini Uingereza kupitia
Mpanga wa Taifa wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele.
Mratibu wa Mpango wa Taifa wa
Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele Dk. Upendo Mwingira akitambulisha wageni
kutoka timu ya Everton na baadhi ya wagonjwa waliotibiwa kupitia mpango
huo kwa ufadhili wa timu hiyo.
Meneja Mradi wa Taasisi ya LSTM
Hayley Mebalsone akizungumzia kuhusu ufadhili wa timu ya Everton kwa
Tanzania katika mpango huo wa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Mabusha na
Matende.
Baadhi ya wagonjwa waliopata tiba na wanaoendelea kupata tima wakiwa katika hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Vida
Mmbaga akiwashukuru wachezaji wa Everton na wagonjwa kwa kukutana na
kushiriki katika hafla hiyo ambayo imewafanya kufahamiana na kujua kazi
kubwa inayofanywa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na
Watoto, Taasisi ya (LSTM) kwa pamoja na timu ya Everton.
Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman
na Mtangazaji wa Televisheni ya Everton Darren Griffiths aliyeinama
wakigawa zawadi kwa wagonjwa walitibiwa na wanaoendelea kutibiwa ugonjwa
wa Mabusha na Matende wakati walipokutana kwenye hoteli ya Seacliff
jijini Dar es salaa. leo.
Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman
na Mtangazaji wa Televisheni ya Everton Darren Griffiths Graham Stuart
pamoja na viongozi kutoka wizara ya Afya pamoja na wagonjwa waliopata
matibabu na wanaoendelea kupata matibabu wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya hafla hiyo.
No comments :
Post a Comment