Jamii Media, CIPESA Wakutanisha Wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ICT
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na
vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania,
lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa
mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya
CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala
Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam
(kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.

Mmoja
wa washiriki katika kongamano hilo, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT
akijadili jambo katika mjadala wa wadau wa ICT, wengine ni Robert
Madziva- Maxcom Africa (kulia) na Chambi Chachage wakiwa katika mjadala
huo.
Mmoja
wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza
kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo.
Kutoka kushoto ni Chambi Chachage-Udadisi Blog, Joseph Ngwegwe-mdau wa
ICT pamoja na Robert Madziva- Maxcom Africa wakiwa katika mjadala huo.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha Abinallah akizungumza na washiriki
wa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT)
nchini Tanzania.
………………………………………………………………………
KAMPUNI ya Jamii Media ya
Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa
kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la
kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini
Tanzania ikiwa ...
ni kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na
mawasiliano pamoja na kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za
wateja wanaotumia huduma hizo.
Akizungumza mara baada ya
kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media,
Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa na matokeo chana baada ya
wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo likiwa kuboresha zaidi
huduma hiyo na usalama kwa watumiaji. Alisema wadau wengi kwenye
kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia
huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za
maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa
huduma za ICT.
Alisema wadau wengi katika
kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (The
Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila ya uwepo wa kanuni jambo
ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na wasimamizi wa sheria husika.
Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media itaendelea kusaidia kutoa mafunzo
kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo bloggers ili
kuona wanakuwa na uelewa na matumizi mazuri ya mitandao yao kupunguza
mkanganyiko kwa wanufaika.
Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji kutoka ‘Compass Communications Ltd’ akiongoza majadiliano kwenye kongamano hilo.Mmoja
wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza
kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo.
Kushoto ni Robert Madziva- Maxcom Africa wakifuatilia mjadala huo.
No comments :
Post a Comment