Kamishna
wa Madini Tanzania Mhandisi Benjamin Mchwampaka akiwa katika picha ya
pamoja na timu wa wataalam wa STAMICO (wanaotekeleza Mradi wa Uchimbaji
Makaa ya Mawe-Kabulo) alipotembelea Mgodi huo hivi karibuni kukagua
maendeleo ya mradi huo ambao ulianza rasmi uzalishaji makaa yam awe
tarehe 30 Aprili, 2017 na kufanikiwa kuzalisha tani 6197 mpaka sasa.
Soko la ndani la makaa hayo linawalenga wazalishaji viwandani hususani
wale wa viwanda vya Saruji (Cement) na watengenezaji wa nguo, pamoja na
magereza na watumiaji wengine wa majumbani.
Shughuli
za Uchimbaji Makaa ya Mawe zikiendelea katika mgodi wa Kabulo Kiwira,
uliopo katika Kijiji cha Kapeta, wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe. Leseni
za Uchimbaji wa Awali wa Madini katika eneo hilo la Kabulo, zina zaidi
ya tani milioni 35 zilizothibitishwa za mashapo ya makaa ya mawe,
yaliyoko karibu na uso wa ardhi, katika mgodi huo wa Kabulo. Mashapo
hayo yanaweza kuchimbwa kwa mfululizo kwa miaka mia moja ijayo.
Mratibu
wa Mradi wa Uzalishaji Mkaa ya Mawe wa Kabulo-Kiwira Bwana Alex
Rutagwelela ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa
STAMICO akielekeza kuhusu zoezi zima la upakiaji makaa ya mawe katika
Malori tayari kwa ajili ya kupeleka katika eneo la mauzo lililopo katika
kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya. Mgodi huo wa
Kabulo-Kiwira uliopo katika kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje mkoa wa
Songwe unamilikiwa na kuendeshwa na STAMICO kwa niaba ya Serikali.
Malori
ya Kampuni ya Lake Cement yakipakia Makaa ya Mawe katika eneo la mauzo
ya makaa hayo, lililopo umbali wa kilometa mbili kutoka katika barabara
kuu ya Mbeya, iendayo nchini Malawi. Eneo hilo la mauzo lipo katika
kijiji cha Kasumulu, Wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya. Makaa hayo ya Mawe
yanazalishwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), katika mgodi wake
wa Makaa ya Mawe wa Kabulo, ulipo katika kijiji cha Kapeta, Wilaya ya
Ileje mkoa wa Songwe.

· Yaanza kuuza makaa hayo kwa kasi
· Yakiri kuwa na akiba ya makaa ya mawe ardhini ya kuchimba kwa zaidi ya miaka mia moja.
Na Koleta Njelekela-STAMICO
Shirika
la Madini la Taifa (STAMICO) limeanza rasmi kuuza makaa ya mawe
yanayozalishwa katika Mgodi wake wa Kabulo ili kukidhi mahitaji ya
watumiaji wakiwemo viwanda vya saruji na nguo na hivyo kukuza Pato la
Taifa.
STAMICO
ilianza uzalishaji wa majaribio wa makaa ya mawe katika mgodi wa Kabulo
uliopo Kijiji cha Kapeta, Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe mnamo tarehe
30 Aprili 2017 na mpaka sasa imeweza kuzalisha tani 6,197.
Akihojiwa
na Mwandishi wa Habari hii, mara baada ya zoezi la uuzaji makaa ya mawe
kuanza rasmi huko Kabulo jana (6 Julai 2017), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa STAMICO Bwana Hamis Komba, amesema Shirika kupitia mradi wake wa
makaa ya mawe wa Kabulo, sasa linaweza kukidhi mahitaji ya watumiaji
wote wa makaa ya mawe nchini, katika kipindi cha miaka mia mfululizo
kutokana na kuwepo kwa mashapo ya kutosha (mineral resources) na nyenye
ubora wa juu katika mgodi huo.
Bwana
Komba amesema matarajio ya Shirika ni kuongeza kiwango cha uchimbaji
makaa ya mawe kutoka tani 600 hadi tani 1000 kwa siku, hatua ambayo
itaiwezesha STAMICO kuzalisha zaidi ya tani 300,000 kwa mwaka.
“Nchi
yetu ina rasilimali nyingi za madini yakiwemo makaa ya mawe, hivyo
tunapenda kuwahikishia wenye viwanda vinavyotumia makaa hayo hususani
viwanda vya Saruji (Cement), kwamba nchi ina makaa ya kutosha hivyo
Serikali haitoshindwa kutosheleza mahitaji na makaa yam awe huku
ikitekeleza kwa vitendo azma yake kujenga Tanzania yenye viwanda, ili
kukuza uchumi wa Taifa" Alifafanua Bwana Komba.
Amewataka
wenye viwanda nchini, kuwasilisha maombi ya kununua malighafi ya makaa
ya mawe, ili STAMICO iweze kuwauzia makaa hayo, ambayo yana viwango vya
ubora vinavyofaa katika uzalishaji wa nishati ya umeme viwandani.
Aidha
Kiongozi Mtendaji Mkuu wa STAMICO amesema hivi sasa Shirika linaendelea
kuimarisha mradi huo wa Kabulo, kwa kuboresha miundombinu, maabara ya
kudhibiti ubora wa makaa na kununua mashine mpya (Crusher) kwa ajili ya
kuponda makaa, kulingana na mahitaji mahususi ya vipimo vinavyhitajiwa
na wateja katika soko.
“changamoto
zilizopo katika utekelezaji wa mradi huu ni pamoja na mtaji mdogo,
mabadiliko ya hali ya hewa hasa nyakati za mvua na ubovu wa kipande cha
barabara yenye urefu wa zaidi ya kilomita 15 kutoka katika eneo la
mgodi, mpaka eneo la mauzo, ambapo barabara hiyo haiwezi kumudu malori
ya zaidi ya uzito wa tani 15 kupita”. alibainisha Bwana Komba.
Awali
Mratibu wa Mradi wa Makaa ya Mawe wa Kabulo-Kiwira Bwana Alex
Rutagwelela, amesema amefurahishwa na matokeo chanya ya mradi huo ya
kufikia hatua ya uuzaji makaa ya mawe, kwani ni fursa nzuri kwa Shirika,
baada ya Serikali kuweka zuio la kuagiza makaa ya mawe kutoka nchi za
nje; wakati nchi ikiwa na makaa mengi ya mawe ardhini.
Amesema
STAMICO kupitia mradi huo, itaendelea kuimarisha viwango vya uzalishaji
wa makaa ya mawe ili kuwafikia wateja wote kulingana na mahitaji yao
“Uwezo
wetu na utaalam katika uchimbaji makaa ya mawe ni wa kimkakati ili
kuweza kukidhi soko la ndani na nje ya nchi. Lengo kuu la mradi huu ni
kutosheleza mahitaji ya kuzalisha umeme wa viwango mbalimbali katika
Mradi wa Umeme wa Kiwira na pia kutosheleza mahitaji ya Viwanda nchini
vikiwemo vya saruji.”
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa STAMICO, Bwana
Deusdedith Magala amewasihi watumishi na wataalam wa Shirika hilo,
kuendelea kujifunga mkanda na kufanya kazi kwa bidii ili kuivusha salama
STAMICO katika kipindi hiki cha mpito, ambapo Shirika linafufua miradi
yake ya uchimbaji madini; itakayoleta mafanikio makubwa na yenye maslahi
mapana kwa Taifa.
Bwana
Magala amesema STAMICO imeweza kuanza uzalishaji wa makaa ya mawe
katika Mgodi wa Kabulo kwa kutumia mtaji mdogo na kubana matumizi; hatua
ambayo imedhihirisha kwamba STAMICO tumethubutu na tunaweza kutekeleza
miradi yetu kwa wakati, pamoja na hali ngumu ya kifedha inayolikabili
Shirika kwa sasa.
“ni
matumaini kuwa katika kipindi cha muda mfupi ujao, watumishi wote
STAMICO tutafurahi, kwani tutaweza kupanua uzalishaji wa makaa ya mawe
huku tukileta matokeo makubwa ya uzalishaji yenye maslahi makubwa kwa
Shirika” Alifafanua Bwana Magala.
Awamu
ya kwanza ya Mradi wa uchimbaji makaa ya mawe wa Kabulo inatekelezwa
kupitia leseni zake mbili za uchimbaji mdogo wa madini Primary Mining
Licences (PMLs) zilizopo ndani ya leseni ya utafiti ya Kabulo zenye
ukubwa wa Hecta 16.52.
Leseni
hizo mbili za Uchimbaji wa Awali wa Madini katika eneo hilo la Kabulo,
zina zaidi ya tani milioni 35 zilizothibitishwa za mashapo ya makaa ya
mawe, yaliyoko karibu na uso wa ardhi, katika mgodi huo wa Kabulo.

No comments :
Post a Comment