Mwanamuziki mkongwe Shaaban
Dede amefariki dunia leo Alhamis Julai 6,2017 saa mbili asubuhi katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu
kwa takriban wiki mbili, mwanae Hamad Dede amethibitisha.
Hamad Dede amesema mipango ya
mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar es salaam,
na kwamba ratiba na taratibu zote zitatangazwa mara zitapokamilika
kupangwa.
Marehemu Dede atakumbukwa kama
mmoja wa wanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania kwa sauti yake tamu na
utunzi wa nyimbo mbalimbali zilizoshika chati akiwa na bendi mbalimbali
zikiwemo Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park na Mondo Ngoma ambako
alikuwa anatumikia hadi maiti yamemkuta.
Chanzo-Michuzi blog
No comments :
Post a Comment