Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu vijana, kazi, ajira na wenye Ulemavu na Mbunge
wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akizungumza wakati alipofungua
kongamano la Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini
leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu vijana, kazi, ajira na wenye Ulemavu na Mbunge wa Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akisalimiana na wajasiriamali mbalimbali mara baada ya kufungua kongamano hilo.
……………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde amesema suala la
kuwainua na kuwapatia elimu ya ujasiriamali wananchi kwa azma ya
kuendesha biashara zao kitaalam na kwa mpangilio utakaokuza vipato vyao kiuchumi ni mkakati endelevu wa kufa na kupona imefahamika.
Mavunde ambaye pi ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu vijana, kazi, ajira na wenye Ulemavu leo alifungua kongamano la Elimu ya Ujasiriamali kwa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kwa kushirikiana na Taasisi ya Mjasiriamali Kwanza.
Katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Cavillam mjini hapa zaidi ya washirikishi 2000 wamepatiwa mafunzo ya kutengeneza bidhaa , kuchota elimu ya ujasiriamali kwa siku nne na baadaye kuunda na kusajili vikundi vya ujasiriamali ambapo ofisi ya Mbunge wa Dodoma Mjini imeahidi kuvitafutia fursa na kuvisimamia.
Alisema kimantiki na kimkakati vikundi hivyo vitapatiwa mbinu za kitaaluma na fursa za kuweza kujipatia mikopo na mitaji ya kufanya shughuli zao, baada ya kujengewa uwezo na kupatiwa elimu kuhusu mafunzo ya ujasiriamali na wajasiriamalu hao
“Tutaanza kugawa kwa vikundi zikiwemo mashine za kutengeneza chaki,mashine ya kutotoleshea mayai (Incubators)za kutengeneza matofali za kunyonyoa manyoya ya kuku (chicken pluckers) za kushonea, zikiwemo na za kukamua juice” Alisema Mavunde.
Aidha alisema pia zitatolewa mashine za kukamlia miwa na za kutengeneza popcorn na zile za kuchapisha yaani (heat press) ambapo jumla gharama za.mashine zote ni shiling milioni 52.
Hata hivyo mbunge huyo alisisitiza kuwa kupitia mpango kazi wa jimbo la Dodoma Mjini, wajasiriamali hao watapatiwa fursa za kukuza vipato vyao kiuchumi na kwa mtu mmoja mmoja na hivyo kujijenga vyema kimaisha baada ya kuchangamkia fursa za uwepo wao katika Makao Makuu ya Serikali Dodoma.
Mavunde ambaye wananchi jimboni mwake akifahamika kwa jina la “De populo Servorum” yaani Mtumishi wa watu, aliahidi atakuwa bega kwa bega na wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa kwa lengo la kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020 pia akishirikiana na mashirika hiari ya kijamii, NGOS na taasisi zinazofundisha masomo ya biashara , utiaji wa elimu na mbinu za kukuza ujasiriamali na watu kujitegemea.
No comments :
Post a Comment