Na. Paschal Dotto- MAELEZO
Serikali ya Awamu ya Tano
inaonyesha dhamira ya dhati ya kujenga Taifa lenye uchumi wa viwanda.
Ujenzi wa viwanda utapunguza ama kuondoa changamoto ya ukosefu wa ajira
hasa...
kwa vijana. Fursa za uwekezaji katika viwanda ni jambo ambalo Mhe.
Rais John Pombe Magufuli amekuwa akilisisitiza katika hotuba zake.
Kwa kuzingatia hilo, wajasiriamali
na wawekezaji wameaanza kujitokeza katika ujenzi na ufufuaji wa
viwanda. Katika makala hii utamwona mtanzania ambaye amebuniu teknolojia
ya kutengeneza mkaa bila kuathiri mazingira.
Mjasiramali huyo ambaye ametumia
fursa hiyo ni Bwana Leonard Gabriel Kushoka ambaye ameanzisha kampuni
ya kutengeneza na kuchakata nishati ya mkaa kwa kutumia mashine maalumu
katika kampuni yake ya Kuja na Kushoka Tools Manufactured Group ambayo
makao yake yako Tabora.
Hii ni teknolojia ya pekee ambayo
utapata nishati ya mkaa bila kuathiri mazingira pia inatoa mwelekeo
mzuri katika kuelekea uchumi wa taifa la viwanda ambayo ni sera ya
Serikali yetu ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. Magufuli , katika kutambua
mchango wa wadau mbalimbali Serikali inaunga mkono kwa yeyote mwenye
fikra pana juu ya teknolojia yeyote anapaswa kutoa wazo.
Kushoka amesema katika upande wa
mazingira kitu kikubwa kinachohitajika ni kuyatunza kwa kuyaweka katika
hali nzuri lakini pia kwa kupanda miti na kuitumia ipasavyo katika
kupata hewa safi.
Katika mkutano wake na waandishi
wa habari jijini Da es Salaam tarehe 12 Julai 2017 Kushoka alikuja na
mashine ambayo kwa hakika ni mashine ya kujivunia kwa Tanzania kuelekea
uchumi wa viwanda. Katika mkutano huu mashine hiyo ambayo kwa lugha ya
kigeni inaitwa “Charcoal Ubiquity” ambayo ina uhakika wa kuzalisha mkaa
bila kuathiri mazingira ya binadamu na watumiaji wa nishati hii muhimu
ilitolewa ufafanuzi.
Kwa mujibu wa takwimu za Wakala wa
Misitu (TFS) Dar es Salaam inatumia magunia 28000 ya nishati hiyo
ambayo ni sawa na tani 1600 kwa siku ambayo ni sawa na asilimia 50 kwa
nchi nzima huku majiji ya Mwanza na Arusha wakifuatia katika takwimu
hizo. Kushoka anasema pia katika kupata nishati hiyo kienyeji inatumia
tani 12 za miti kwa tani 1 moja ya mkaa kwa hiyo kwa takwimu hizo za Dar
es Salaam zinaonyesha ni jinsi gani uharibifu wa mazingira unatokea
katika misitu asili ya nchi yetu.
Katika matumizi sahihi ya
teknolojia hii ya Kushoka Tools Manufactured Group ni kujivunia kwa
nchi yetu kuelekea kutimiza sera ya awamu ya tano inayoelekea kuijenga
Tanzania ya viwanda , mashine hii yenye kutumia takataka za aina yeyote
ikiwemo mabaki ya mazao isipokuwa plastiki katika kuzalisha mkaa kwa
matumizi ya nyumbani
Katika teknolojia yake Bwana
Kushoka alisema mashine hii ina uwezo wa kuzalisha wastani kilo 160 kwa
saa moja , pia inahitaji watu 7 katika ufanyaji kazi wake ambao
wanahitajika kwa kuiwezesha katika kuchakata nishati hiyo ya mkaa, na
ina uwezo wa kutoa magunia 20 kwa siku jambo ambalo linarahisisha maisha
na matumizi ya nishati hiyo majumbani.
Katika ufumbuzi huu ambao pia
utakuwa bora kwa kutoa ajira kwa vijana kwani katika viwanda vidogo
vidogo vitakvyoanzishwa vitakuwa na watumishi na kusaidia kuondoa kero
ya ajira kwa vijana
Bwana Kushoka anasema kuwa
malighafi zinazotumika katika mashine hiyo ni takataka za aina yoyote
isipokuwa vitu vya plastiki, kwa hiyo kwa watumiaji wa mashine hii
wanapaswa kujua kuwa plastiki siyo malighafi ya mashine hii. Kwa takwimu
za mazingira jiji la Dar es Salaam linazalisha tani 5000 kwa siku kwa
hiyo ni vyema teknolojia hii ikatolewa kwa elimu kubwa ili kusaidia
utunzaji wa mazingira.
Katika matumizi ya mashine hii ni
kitu ambacho ni muhimu zaidi katika kutumia teknoljia hii, zaidi mashine
hii ya kujivunia kwa nchini yetu inatumia nishati ya mafuta ya diseli
na umeme lakini sanasana inategemea na maamuzi ya mtumiaji au mnunuzi wa
mashine hii, ila kwa wale walioko vijijini ambako hasa nishati ya umeme
haipatikani kirahisi wanashauriwa kupata mashine itumiayo diseli ili
kuepusha usumbufu wa matumizi ya teknolojia hii.
Akizungumzia mabaki ya mazao
kutoka mikoa ambayo huzalisha mazao mbalimbali ikiwemo tumbaku, karanga,
mpunga, mahindi, Kushoka alitaja baadhi ya mikoa hiyo kuwa ni Tabora,
Shinyanga, Mwanza na Rukwa. Maeneo hayo yanapswa kupata teknolojia hiyo
ikizingatiwa malighafi inapatikana kiurahisi na kutumika katika
kuchakata mkaa hatua ambayo inasaidia kutunza uoto wa asili nchini.
Katika matumizi ya mashine hii ni
kitu ambacho ni muhimu zaidi katika kutumia teknoljia hii, zaidi
mashine hii ya kujivunia kwa nchini yetu inatumia nishati ya mafuta ya
diseli na umeme lakini sanasana inategemea na maamuzi ya mtumiaji au
mnunuzi wa mashine hii, ila kwa wale walioko vijijini ambako hasa
nishati ya umeme haipatikani kirahisi wanashauriwa kupata mashine
itumiayo diseli ili kuepusha usumbufu wa matumizi ya teknolojia hii.
Kwa Dar nes Salaam tayari kuna
vituo vinne ambayo elimu kuhusu teknolojia hii ishatolewa vituo kama
Pugu, Tandika, Tegete pamoja na Mbezi Kimara kwa hiyo kwa wakazi wa jiji
la dar es salaam wanatakiwa kutembelea vituo hivyo kwa elimu na kupata
mashine hiyo yenye teknoljia ya kisasa
Kwa watanzania wote tunatakiwa
kuunga mkono jitihada hizi kubwa zinazo fanywa na kuja na kushoka tools
manufactures group, kwa kununua mashine kwa matumizi kuchakata mkaa na
kutunza mazingira kwa usafi wa nchi yetu kwa maendeleo ya taifa, kupata
mashine hii ya kujivunia katka mapinduzi ya viwanda inategemea na
mahitaji ya mnunuzi kwani mashine hii inauzwa kuanzia shilingi milioni 3
mpaka milioni 15 kutokana na maamuzi lakini bila kusahau matumizi ya
mtumiaji katika teknolojia hii ya kisasa.
Taifa letu, serikali ni yetu,
mistu ni yetu tunatakiwa kutumia mazingira vizuri kwa kupanda na kutunza
mistu yetu ,nunua mashine ya kuchakata mkaa ili kuepusha ukataji miti
ovyo na kuharibu mazingira.
No comments :
Post a Comment