Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akipokelewa na Kamishna Jenerali
wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala, wakati kiongozi huyo alipokua
anawasili Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA), mjini Moshi kwa ajili
ya kukabidhiwa vifaa vya Tehama vilivyotolewa na Ubalozi wa China nchini
kwa ajili ya matumizi ya chuo hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (kulia) wakipokea moja ya kompyuta
kutoka kwa Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (wapili kushoto)
katika hafla ya makabidhiano ya vifaa msaada vya Tehama vyenye thamani
ya shilingi milioni 33 vilivyotolewa na Ubalozi huo kwaajili ya
kukisaidia Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo mjini Moshi.
Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Maurice Kitinusa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia-waliosimama)
akishuhudia Balozi wa China nchini, Dk. LU Youqing (kushoto) na Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala walipokua wakitia saini
Mkataba wa Makabidhiano wa msaada wa vifaa vya Tehama vilivyotolewa na
Serikali ya China kwa ajili ya Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA),
kilichopo mjini Moshi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (kushoto), Balozi wa China nchini,
Dk. LU Youqing (aliyevaa saa) pamoja na maafisa wengine wakimsikiliza
Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA),
Mkaguzi wa Uhamiaji, Zawadi Chazuka alipokua anawaonyesha kifaa cha
kuangalia alama au maandishi ambayo hayawezi onekana kwa macho ya
kawaida mpaka kifaa hicho kitumike. Ubalozi wa China ulitoa msaada wa
vifaa vya Tehama vyenye thamani ya shilingi milioni 33 kwa ajili ya
matumizi ya chuo hicho kilichopo mjini Moshi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji (CGI), Dkt. Anna Makakala (watatu kushoto), Balozi wa China
nchini, Dk. LU Youqing (watatu kulia), Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa
Uhamiaji na Ujumbe kutoka China mara baada ya Balozi wa China kutoa
msaada wa vifaa vya Tehama kwa ajili ya matumizi ya Chuo cha Uhamiaji
cha Kikanda (TRITA)
No comments :
Post a Comment