NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
OFISI nyingi za Mamlaka ya Mapato
nchini, (TRA), habari kubwa ni "kodi ya majengo", hii ndiyo habari ya
mjini hata huku mitaani. Idadi kubwa ya watanzania wameamua kwa hiari
yao na hata kumshangaza Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kujitokeza kwa
wingi kulipa kodi" Katuka historia ya nchi hii haijapata kutokea kuona
watanzania tena kwa hiari yao wenyewe, wakiwa kwenye misururu mirefu
wakisubiri kulipa kodi, hili ni jambo zuri na nimefurahishwa pia na TRA
kuongeza muda wa kulipa kodi hiyo" Alisema Rais Magufuli wakati
akifungua rasmi maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam
Julai 1, 2017.
Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuona
mwitikio wa wananchi kuwa mkubwa sana katika ulipaji wa kodi hiyo ya
majengo, iliondoa tarehe ya mwisho ya kulipa kodi kutoka Juni 30, 2017
na kuongeza wiki mbili zaidi hadi Julai 15, 2017 na hivyo kutoa fursa
kwa wananchi kulipa kodi hiyo. Katika viwanja vya maonesho ya 41 ya
biashara yakimataifa ya Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa wkenye foleni
wakisubiri kuhudumiwa kwenye banda la TRA, lililoko viwanja vya Mwalimu
Nyerere maarufu "viwanja vya sabasaba" barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam leo Julai 3, 2017
Mwananchi huyu akihudumiwa na afisa kodi wa TRA, Bi.Witness Msaki(kulia)
Afisa kodi wa TRA, Bi.Witness Msaki, akipitia kumbukumbu za mwananchi aliyefika kupatiwa huduma
Afisa kodi wa TRA, Bi.Judith Lwaikondo, akizungumza na mwananchi
Afisa kodi wa TRA, Bi.Salome Charles,
(kushoto), akizungumza na wananchi waliofika banda la TRA ili kulipia
kodi ya majengo leo Julai 3, 2017.
Bi Levina Shirima, Afisa Kodi TRA, akiwa kazini
Bi.Salome, (kushoto), akimsikiliza mwananchi
Bi. Judith Lwaikondo, Afisa kodi TRA akimuhumia mwananchi
Afisa kodi wa TRA, Bw.Ananias Kimbi, (kushoto), akimuhudumia mwananchi
No comments :
Post a Comment