Win-God Simon, (kushoto), Afisa wa PSPF
akiwahudumia wananchi na wanachama wa Mfuko huo waliotembeela banda la
PSPF leo Julai 6, 2017
MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaahidi
wananchi wanaojitokeza kwenye banda la Mfuko huo, lililoko jengo la
Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu
kama Sabasaba, kuwa wataendelea kupatiwa huduma zote kama ambazo
wamezoea kuzipata kwenye ofisi za Mfuko huo kote nchini.
Ahadi hiyo imetolewa leo Julai 6, 2017
na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, baada ya
kuona umati mkubwa wa wananchi waliofika kupatiwa huduma mbalimbali
zikiwemo zile za wanachama kujua michango yao, wananchi kujiunga na
mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), ambapo mtu aliyejiunga na mpango
huo husajiliwa na kupatiwa kitambulisho papo kwa hapo. "Leo idadi ya
watu imeongezeka sana bila shaka wamevutiwa na huduma zetu na
tunawahakikishia tutaendelea kutoa huduma bora na za haraka hadi tarehe
ambayo maonesho haya yatafikia kilele kama alivyoagiza Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa siku za
maonesho zimeongezeka hadi Julai 13, 2017 badala ya Julai 8." Alifafanua
Bw. Njaidi.
Idadi kubwa ya wananchi waliofika kwenye
banda hilo ni wale wajasiriamali ambao wengi wamejiunga na mpango wa
uchangiaji wa hiari ambapo moja ya faida kubwa ya kujiunga na mpango huo
ni kupata fao la bima ya afya inayomuwezesha mwanachama kupatiwa
matibabu yeye na wategemezi wake kwenye hospitali zilizoaishwa kote
nchini.
Wananchi waliofurika wkenye banda la PSPF, leo Julai 6, 2017
Bw. Costa wa PSPF, (kushoto), akifafanua jambo kwa wananchi hawa waliofika kwenye banda la PSPF
Afisa Michango wa PSPF, Bw. Noah Amri,
(kushoto), na Afisa Uendeshaji anayeshughulikia mpango wa uchangiaji wa
hiari (PSS), Bi. Asmahan H. Haji, wakiangalia taarifa kwenye kompyuta.
Afisa msaidizi wa uendeshaji Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Musa Mfaki(kushoto), akimuhudumia mwananchi
Mhandisi Ally Shanjirwa wa PSPF, (kulia), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la PSPF
Wananchi waliofurika wkenye banda la PSPF, leo Julai 6, 2017
No comments :
Post a Comment