Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa
Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge wakati wa uzinduzi wa
mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli
mbiu “Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha
Maendeleo”iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohamoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi wa
mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli
mbiu “Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha
Maendeleo”iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021
wenye kauli mbiu “Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha
Maendeleo”iliyofanyika kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es
Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu maalumu
chenye mpango mkakati wa Water Aid
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu maalumu
chenye mpango mkakati wa Water Aid uliozinduliwa kwenye kwenye hotel ya
HyattRegency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana leo ...
amezindua Mpango Mkakati wa Water AID Tanzania .
Katika mkutano huo uliofanyika
kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge, Naibu Waziri
wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Mkurugenzi wa Water Aid
Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Olutayo Bankole –Bolawole,Mkurugenzi
WaterAid Tanzania Dkt. Ibrahim Kabole na wadau mbali mbali wa maji, afya
na mazingira.
Mpango Mkakati wa miaka mitano wa
Water Aid Tanzania wenye lengo la “ Kuweka Maji Safi na Usafi wa
Mazingira (WASH)” katika mipango ya Maendeleo ya Jamii.
Makamu wa Rais aliwapongeza
Water Aid Tanzania kwa mpango wake huo, alisema Maji ni rasilimali
ambayo haijawahi kutosheleza mahitaji ya dunia na hapa kwetu pia kwani
kuna mahitaji makubwa ya maji kwa ajili ya shughuli za kijamii, kiuchumi
na kuhuisha na kutunza mazingira.
Vilevile vyanzo vya maji
vinaathiriwa sana na Ukame,kufurika n, kuvuruga mtiririko asilia,
mabadiliko ya hali ya hewa ongezeko la idadi ya watu na viumbe wengine
(Wanyama).
Mpango wa Water Aid Tanzania wa
miaka mitano utawezesha kuiweka Tanzania kwenye ramani ya matumizi
endelevu ya rasilimali ya maji na utachangia katika utekelezaji wa
malengo tuliyojiweka ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa
wananchi kulingana na Sera yetu ya Maji na pia kutekeleza ahadi
tulizozitoa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya 2015.
Makamu wa Rais alisema Serikali
kwa kushirikiana na wadau mbali mbali imeendelea kuboresha hali ya
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini
ambapo utekelezaji huo umeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa
huduma ya maji vijijini ambapo kwa mwezi Juni 2017 jumla ya watu
22,952,371 sawa na asilimia 72.58 ya wananchi waishio vijijini wanapata
maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kama sera ya maji ya
mwaka 2002 inavyoelekeza huku katika Miji Mikuu ya mikoa kutoka
asilimia 86 hadi asilimia 95, katika miji mikuu ya Wilaya , miji midogo
na miradi ya Kitaifa kutoka asilimia 60 hadi asilimia 75 na katika jiji
la Dar es Salaam kutoka asilimia 72 hadi asilimia 95 ifikikapo 2020.
Makamu wa Rais alisisitiza suala
la usafi wa mazingira na kuhakikisha tunalinda afya zetu tusishambuliwe
na magonjwa ya milipuko kama vile kipindu pindu na homa za matumbo.
“Sote tunajukumu kubwa kuhakikisha tunapata maji na kuzungukwa na
Mazingira safi”.
Makamu wa Rais aliwaagiza
wanaohusika na usimamizi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira
kuongeza jitihada zaidi ifikapo 2020 idadi ya wananchi wanaopata maji
iwe imeongezeka kufikia malengo tuliyojiwekea.
Mwisho, Makamu wa Rais
aliwashukuru wawakilishi wa mashirika yote ya Maendeleo, wafadhili
binafsi na Watendaji wengine ikiwa pamoja na Sekta Binafsi na Taasisi za
Kidini ambazo zimesaidia katika upatikanaji wa huduma za maji na usafi
wa mazingira na kuboresha mazingira.
No comments :
Post a Comment