Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa
Samwel Manyele (kulia) akimsikiliza Afisa wa Polisi aliyetembelea Banda
la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuweza kufahamu huduma
mbalimbali zinazotolewa na Maabara zilizopo chini ya Ofisi yake kwenye
Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) yanayoendelea kwenye
Viwanja vya Saba Saba, Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda
ya Mashariki, Bi. Everlight Matinga (wa pili kulia) akimfahamisha
mwananchi aliyetembelea Banda la Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali huduma zinazotolewa na Maabara za Wakala kuanzia Makao Makuu na
Kanda zake Sitazilizoko kwenye Mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dar es
Salaam, Mtwara na Dodoma.
Mtumishi wa Wakala wa Maabara ya
Mkemia Mkuu wa Serikali, Bi. Lulu Kiwia (kulia) akimueleza mwananchi
aliyetembelea Banda la Wakala huduma zinazotolewa na Maabara ambazo
zinahusiana na maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida pia huduma
ambazo Wakala inatoa moja kwa moja katika kutekeleza majukumu yake kwa
Serikali.
Kaimu Meneja wa Masoko na Huduma
kwa Wateja, Bw. Cletus Mnzava (wa pili kulia) akimfahamisha mwananchi
aliyetembelea Banda la Wakala shughuli mbalimbali zinazofanywa na
kuratibiwa na Maabara zilizoko chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa
Serikali. Kushoto ni Mtumishi wa Wakala, Bw. Sabas Mandari, akisikiliza.
No comments :
Post a Comment