| Ofisa Masoko kutoka Kampuni ya CFAO Motors Ltd, Angelina Ndege akizungumza katika mkutano huo kuhusu kudhamini tamasha hilo. |
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Idara ya Kuunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kuhamasisha
washiriki kuhudhuria kwa wingi katika tamasha kubwa la muziki ambalo
halijawahi kushuhudiwa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Malipo wa
kwa Tigo Pesa, Newton David na Meneja Masoko wa TBLKitengo cha Bia Laini Afrika Mashariki, Amou Majok.
Mratibu wa Malipo wa kwa Tigo Pesa, Newton David (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Meza kuu.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wasanii wa hapa nchini watakaotoa burudani katika tamasha hilo. Kutoka kulia ni Vanessa Mdee, Nareel Mkono na Aika Marreale.
Na Dotto Mwaibale
KAMPENI
ya Castle lite unlocks inahamasisha washiriki kuhudhuria kwa wingi
katika tamasha kubwa la muziki ambalo halijawahi kushuhudiwa Tanzania.
Wito
huo umetolewa na Meneja wa mahusiano ya wateja wa kampuni ya Tanzania
Brewaries Limited (TBL) kwa Afrika Mashariki, George kavishe katika
taarika yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, ambapo
alitumia fursa kuwataja wadhamini na wabia wa kampeni hiyo.
“Kwa
mara nyingine tena tunawakumbusha wapenzi wa muziki, hasa walioko katika
jiji la Dar es salaam na maeneo ya karibu kujiandikisha kwa wingi kwani
tukio hilo la aina yake linakaribia” alisema Kavishe, akiongeza kuwa
washiriki watapata fursa adimu sana ya kufurahia bonanza lamuziki
litakalo tayarishwa na brand ya kipekee ya bia, Castle Lite hivi
karibuni.
Akitangaza
washirika, kavishe alipongeza mchango wao, akisema kwamba wametekeleza
jukumu kubwa katika mafanikio ambayo kampeni hiyo imefikia mpaka sasa.
Alitaja
wadhamini kama vile Tigo Tanzania (mshirika rasmi wa mawasiliano ya
Simu), Clauds FM (Mshirika kama chombo cha habari), CFAO Motors
(Mshirika katika usafirishaji), Marlborona Serena Hotel Dar es Salaam
(Mshirika katika malazi).
“Tunawashukuru
sana washirika wetu kwa kukamilisha juhudi zetu katika kuelekea kwenye
tamasha la nne la muzikiambalo linahakika kuwa litakuwa ni chanzo cha
mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki wa wandani”, Kavishe amesema
kuhusu Bonanza kubwa ambalo limepangwa kufanyika tarehe 22 mwezihuu wa
julai katika ukumbi wa Leader’s Club hapa Dar es salaam.
Kwa
mujibu wa Kavishe, kampeni ya Castle Lite Unlocks ni harakati kubwa
ambapo bia ya Castle Lite imekuwa inabadilisha mwelekeo wa mchezo
kwa kuleta wasanii wakubwa na mashuhuri wa imataifa kuja kufurahia
pwani za Afrika kwa kutoa burudani ya kipekee ya ‘Extra Cold’ katika
tamasha kubwa la‘Castle Lite Unlocks’
“Tamasha
la mwaka huu litakuwa na neema ya kutembelewa na wanamuziki maarufu na
wakongwe wa Hip Hop, huku wanaochipukia wakiwa wanasindikizwa na
wanamuziki maarufu wanaotikisa bongo flava Tanzania wakiongozwana
Diamond Platnumz” alisema Kavishe, akiwataja wasanii wengine watakao
kuwepo kuwa ni, Casper Nyovest Kutoka Afrika kusini, Vanessa Mdee, kundi
la Weusi na Navy Kenzo ambao ni wa hapa hapa nchini Tanzania.
Kavishe
alishauri wapenzi wamuziki kununua tiketi kupitia Tigo Pesa namba 0674
444 444 na kwenda kuzichukua katika Tigo Shop yoyote hapa Dar es salaam.
Mitandao mingine ya simuinaweza kununua tiketi kwa kuchagua
“mitandaomingine” katika menyu ya simu pesa zao na kununua kwa kupitia
namba hiyo hiyo ya malipo.
“Manunuzi
ya tiketiyanaenda kwa kasi sana kwa hiyo ni na wasisitiza watu wote
kununua tiketi zao sasa kwa sababu hii ni tukio ambalo haupaswi kukosa.
Castle Lite ni bidhaa bora ambayo inakuletea uzoefu wa hali ya juu.
Watu
wategemee burudani ambayo haijawahi kutokea hapa Tanzania, tumeandaa
tamasha hili kwa hali ya juu, kiwango cha usalamani cha hali ya juu na
mpangilio wakipekee wa ukumbi wa tamasha ambao utawaacha watu wakiwa
katika hali ya mshangao” alisema Kavishe.
“Gharama
ya tiketi ni Tshs 20,000 akini watejawatakaol ipa kwa Tigo Pesa
watafurahia punguzo la bei la Tshs 5,000, hivyo watalipa Tshs 15,000
kwatiketi moja,” alisema Kavishe, huku akiongeza kwamba wateja wataweza
kujipatia tiketi zao kutoka katika maduka ya huduma kwa wateja ya Tigo
(Tigo shop) yaliyopo karibu nao.
Alizitaja
sehemu ambalko wanaweza kwenda kuchukua tiketi zao kuwa ni pamoja na:
Mlimani City-Mlimani City Mall, Makumbusho (mkabala na), Palm Beach
Residence-Ocean Road, Nkurumah- Nyerere Road- Gold Star,
Buguruni-Rozana, Quality Center-Quality Center Mall, JM Wall- Hotel
Harbor View, Masaki- Haille Selassie Road, Kariakoo-Msimabazi/Pemba
Street, Manzese Darajani, Kigamboni-Ferry, Tegeta-Kibo Complex na
Mbagala- Oil Com Gas Station.
Kwa
upande mwingine, Kavishe aliongeza kwamba wateja pia wanaweza kupata
tiketi kwa pesa taslimu Sh 20,000/= katika maeneo yafuatayo, Clouds
Fm-Mikocheni, Funzone Shamo Tower-Mbezi Beach, Leader’s Club-Kinondoni
na duka la Bron to Shine-Mwenge.
Kampeni
ya Castle lite Unlocks itahudhuriwa na washindi 22 kutoka Zambia na 19
kutoka Tanzania ambao wamejishindia tiketi za “kiwango cha VIP” ambayo
itawapatia fursa ya kusafirishwa kwa ndege mpaka Jijini Dar es salaam,
kukaa katika hotel maarufu kwa siku mbili, kufurahia burudani ya hali ya
juu, kupelekwa na kurudishwa kutoka katika tamasha wakati huo huo ukiwa
unapokea huduma za VIP kwa wakati wote.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
No comments :
Post a Comment