Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Ndugu Salehe Muhando (Wa tatu) kushoto akitoa taarifa ya Wilaya yake kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani(Katikati) wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya
barabara na madaraja Mkoani Katavi.
Meneja wa Wakala wa barabara (
TANROADS) Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi (Wa tatu kulia) akifafanua
ramani ya mtandao wa barabara iliyopo katika Wilaya ya Tanganyika kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani
(Kushoto) wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya barabara na
madaraja Wilayani hapo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia) akipokea maelezo
kutoka Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Katavi Eng. Abdon
Maregesi (Wa pili kulia) wakati alipotembelea kambi ya Mkandarasi
anayejenga barabara ya Mpanda -Vikonge (35KM) Kwa kiwango cha lami
Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akitoa maelekezo Meneja wa
Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi (Wa
pili kulia) wakati alipokagua barabara ya Mpanda -Vikonge (35KM) ,
Ifukutwe – Mwese (Km 109) na Mwesi hadi Mto Lugosi mpakani mwa katavi
na kigoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akielekea kukagua Daraja la Lugosi
ambalo ujenzi wake umekamilika, Daraja hili linaunganisha Wilaya ya
Tanganyika na Uvinza.
……………………………………………………………………
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amemtaka Meneja wa wakala wa Barabara
nchini (TANRODS) mkoa wa Katavi na Tanroads mkoa wa Kigoma kushirikiana
ili Kuunganisha Wilaya ya Tanganyika na Uvinza kwa Barabara za kiwango
cha
changarawe ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wilaya hizo.
Naibu Waziri Ngonyani ametoa
agizo hilo baada ya kukagua ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya
Mpanda -Vikonge (35KM), Ifukutwe – Mwese (Km 109) na Mwesi hadi Mto
Lugosi mpakani mwa katavi na kigoma.
“Ni wakati muafaka sasa kufungua
Barabara hizi hadi ukanda wa Ziwa Tanganyika ili kurahisisha usafiri kwa
wananchi kwa njia ya barabara baada ya kuwepo changamoto ya usafiri wa
majini kupitia Meli ambazo kwa sasa ni chache hivyo kukamilika kwa
miradi hiyo kutafanya uwepo wananchi wawe na usafiri wa uhakika,”
amesema Eng. Ngonyani.
Ameongeza kuwa serikali itachukua
hatua za haraka kuhakikisha wanachi wa Wilaya ya Tanganyika wanakuwa na
barabara za uhakika zitakazorahisisha usafirishaji wa mazao na hivyo
kupandisha thamani ya mazao hayo kwa wananchi.
Kwa upande wake Meneja wa
TANROADS Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi amemuhakikishia Waziri
Ngonyani kuwa atahakikisha barabara hizo zinafanyiwa matengezo ya mara
kwa mara ili kuzifanya zipitike kwa urahisi katika vipindi vyote vya
mwaka.
Kwa upande wa huduma za
mawasiliano ya simu, Eng. Ngonyani amesema Wizara yake itashirikiana na
kampuni za simu zilizopo nchini pamoja na mfuko wa mawasiliano kwa wote
(UCSAF) ili kuhakikisha sehemu ambazo hazina mawasiliano ya huduma za
simu ya uhakika zinapata mawasiliano.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Katavi
Ngugu, Saleh Mhando amesema kukamilika kwa Barabara hizi kutafungua
fursa za kibiashara na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa pande mbili
za wilaya ya uvinza na Tanganyika.
“Wananchi wa Wilaya hizi hufanya
shughuli za uvuvi hivyo kuimarisha kwa barabara hizi kutarahisisha
usafirishaji wa samaki kufika katika masoko kwa wakati na hivyo kukuza
kipato cha wananchi wa ukanda huu wa ziwa Tanganyika,” amesema Mhando.
Naibu Waziri Eng. Ngonyani yupo
katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya Ndege,
Ujenzi wa Nyumba za viongozi na Madaraja katika Mkoa wa Katavi.
No comments :
Post a Comment