Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, Bw. Adam Mayingu, aliongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi.
Neema Muro na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji Bw. Gabriel Silayo,
baada ya kufungwa kwa semina kwa wastaafu watarajiwa wa wilaya zote za
mkoa wa Mwanza iliyofanyika ukumbi wa chuo cha watumishi wa Benki Kuu ya
Tanzania, huko Capri-point jijini Mwanza.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Katika
hotuba yake aliyotoa Kati wa ufunguzi rasmi wa semina hiyo, Bw.
Mayingu alisema, PSPF inatarajia kulipa wastaafu kiasi cha shilingi
Trilioni 1.3 kwa mwaka huu tu wa 2017/18."Kwa mwaka 2017/18 pekee, Mfuko
unatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia
shilinginTrilioni 1.3.Kisai hiki cha Mafao ni kikubwa, hivyo kupitia
semina hii Wastaafu watarajiwa wa PSPF wamejifunza namna ya kupanga
maisha yao baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji wa
mafao yao ili mafao haya yaweze kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya
uchumi na kuongeza fursa za ajira." Alisema Bw. Mayingu katika hotuba
yake. Miongozi mwa mambo waliojifunza wastaafu hao wanaokadiriwa kufika
450, ni pamoja na uanzoshwaji wa viwanda vidogo vidogo, namna bora ya
utunzaji fedha kwenye taasisi za fedha, (mabenki), lakini pia mbinu
mbalimbali za ujasiriamali. Bw. Kuhsu mafunzo yaliyotolewa na SIDO, Bw.
Mayingu alisema Mfuko ulikutana na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo
vidogo (SIDO) na kujadiliana namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza
kushirikiana na kuwafanya wastaafu wa PSPF wapate ujuzi wa kuwekeza na
kuweza kutengeneza ajira kwa vijana. "Lengo likiwa SIDO iwajengee uwezo
kitaalamu na kuwapatia vifaa ili wastaafu wa PSPF waweze kuanzisha
viwanda vidogo vidogo na shughuli nyingine za uzalishaji." Alisema Bw.
Mayingu. Alisema wameamua kufanya hivyo kwa kzuingatia ukweli kuwa,
katika kufuatilia wastaafu wa Mfuko wamegundua kuwa baadhi yao
hujiingiza katika biashara mbalimbali ambazo hawakujiandaa vema na
matokeo yake kupoteza mafao yao.
Washiriki wakijadiliana
Mkurugenzi wa Masoko wa wa Mfuko wa
uwekezaji wa pamoja UTT-AMIS, Daudi Mbaga, akitoa mada ya namna
wanachama wa taasisi hiyo wanavyoweza kufaidika kwa kuwekeza kwenye
Mfuko huo.
Mshiriki akizungumza kwenye semina hiyo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili
Mmoja wa wastaafu wa PSPF, ambaye kwa
sasa ni mteja wa benki ya NMB, akitoa ushuhuda jinsi alivyofaidika baada
ya kuitumia benki hiyo pale alipostaafu ambapo sasa anaedesha miradi
mbalimbali kufuatia mikopo anayompewa na benki hiyo na kumfanya aishi
maisha ya amani.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam
Mayingu, (kushoto), Mkurugezni wa Uendeshaji, Bi.Neema Muro, (katikati)
na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Silayo, wakifurahia
michango ya mawazo kutoka kwa washiriki wa semina.
Meneja wa Mfunzo kutoka Shirika la
Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo SIDO, Bi. Beata Minga, (kulia),
akiongoza kikao wakati wa kufungwa kwa semina ya siku mbili ya mafunzo
kwa wastaafu watarajiwa
Mshiriki akichangia mawazo yake kwenye semina hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam
Mayingu, (katkati), akiwa na viongozi wengine wa Mfuko kutoka kushoto ni
Meneja Mipango na Utafiti, Bw.Luseshelo Njeje, Mkurugenzi wa
Uendeshaji, Bi. Neema Muro, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw.
Gabriel Sulayo, na Meneja wa Pensehini za Wastaafu, Bw.Mohammed Salim.
Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambaye awali
aliifungua rasmis semina hiyo, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, (watatu kulia waliokaa),
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw.John Mongella, (watatu kushoto), Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (wapili kulia), na Kaimu Mwenyekiti wa
Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, viongozi wengine na
wafanyakazi wa PSPF
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini
wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
PSPF, Bi. Neema Muro wakiwasili ukumbini
Naibu waziri wa fedha na mipango, Dkt.
Asshatu Kijaji, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw.
Nyakimuro Muhoji (katikati) na Mkurugenzi Mkuu, Bw. dam Mayingu
wakiwasili ukumbini.
No comments :
Post a Comment