Mkuu wa
operesheni za polisi, naibu kamishna DCP Liberatus Sabas, akionyesha bunduki
aina ya smg zilizopatikana juzi usiku wakati wa mapambano ya kurushiana risasi
baina ya wahalifu na polisi katika kijiji cha pagae wilayani kibiti mkoani
pwani. bunduki 2 aina ya smg zilipatikana pamoja na magazini 2 na risasi 17.
picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.
NA FRANK GEOFRAY-JESHI LA POLISI.
JESHI la Polisi nchini limefanikiwa
kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha
mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu
kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.
Akielezea tukio hilo Mkuu wa
Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas
alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku
kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi
wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita
ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na
kuanza kuwarushia risasi Polisi.
Sabas alisema baada ya hali hiyo
kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya
nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao
baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.
“Katika tukio hilo tumefanikiwa
kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17
zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri
na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama
katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.
Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu
wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na
usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo
yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.
Vilevile amewataka wananchi kutoa
taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila
mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha
kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
No comments :
Post a Comment