Mratibu wa Mpango Kabambe wa
Kuboresha na Kuimarisha Takwimu nchini (Tanzania Statistical Master
Plan-TSMP) kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Philemon Mahimbo
akiwasilisha mada wakati wa mafunzo kwa wanasheria kuhusu sheria mpya ya
Takwimu ya Mwaka 2015 yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
Meneja wa Idara ya Mbinu za
kitakwimu, Viwango na Uratibu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Emilian
Karugendo akiwasilisha mada kuhusu takwimu na takwimu rasmi wakati wa
mafunzo kwa wanasheria kuhusu sheria mpya ya Takwimu ya Mwaka 2015
yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
Baadhi ya wanasheria kutoka Wizara
na taasisi za Serikali wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada
zinazohusu sheria mpya ya Takwimu ya Mwaka 2015 wakati wa mafunzo kwa
wanasheria kuhusu sheria hiyo yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
Baadhi ya wanasheria kutoka
Wizara na taasisi za Serikali wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa
mada zinazohusu sheria mpya ya Takwimu ya Mwaka 2015 wakati wa mafunzo
kwa wanasheria kuhusu sheria hiyo yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
………………………….
Na: Veronica Kazimoto
Morogoro
02 Juni, 2017.
Uratibu wa Mfumo wa Taifa wa Takwimu umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha uzalishaji takwimu rasmi nchini.
Hayo
yamebainishwa na Mratibu wa Mpango Kabambe wa Kuboresha na Kuimarisha
Takwimu nchini, Philemon Mahimbo wakati wa mafunzo kwa Wanasheria wa
Wizara na
Taasisi za Serikali kuhusu Sheria mpya ya Takwimu No. 9 ya
Mwaka 2015 yaliyofanyika leo mkoani Morogoro.
Mahimbo
amesema mfumo huu unaoratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mujibu
wa Sheria ya Takwimu Na 9 ya mwaka 2015, umeweza kusaidia upatikanaji wa
takwimu rasmi ambazo zinatumika katika kupanga na kutekeleza miradi
mbalimbali ya kimaendeleo na kupunguza changamoto ya kukinzana kwa
takwimu zilizokuwa zinatolewa na taasisi mbalimbali.
Kwa
upande wake Mwanasheria wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Oscar Mangula
amesema Sheria mpya ya Takwimu No. 9 ya Mwaka 2015 haimzuii mtu ama
taasisi kufanya utafiti bali inamtaka mtu au taasisi kuwasiliana na
Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupata kibali na miongozo kama anataka takwimu
anazozikusanya ziwe rasmi.
“Sheria
hii mpya ya Takwimu No. 9 ya Mwaka 2015 sio kwamba inazuia watu ama
taasisi kuendesha shughuli za utafiti au za kukusanya takwimu kwa
matumizi ya mtu binafsi au taasisi husika nchini bali inawataka kutumia
miongozo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili takwimu wanazozikusanya
ziwe rasmi,” amesema Mangula.
Oscar
Mangula amebainisha kuwa ni kosa kisheria kwa mtu ama taasisi kuendesha
utafiti wenye miongozo isiyothibitishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na
kuzitangaza kama takwimu rasmi.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imepewa mamlaka kisheria ya kuratibu, kusimamia, kuchambua na kusambaza takwimu rasmi nchini.
No comments :
Post a Comment