Mkuu
wa Kitengo cha Udhibiti na Mahusiano na Serikali wa Kampuni ya simu za
mkononi ya Tigo, Sylvia Balwire akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani
ya Sh 110 milioni kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT Erwin
Telemans, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye
ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mama mwenye mtoto mwenye ugonjwa wa miguu pinde akizungumza na vyoombo vya habari mara baada ya makabidhiano ya hundi yenye thamani ya Sh 110 milioni kwa hospitali ya CCBRT, fedha hizo zimetolewa ili kusaidia matibabu kwa watoto wenye ugonjwa wa miguu pinde, hafla hiyo ilifanyika mapema leo jijini Dar es Salaam. |
…………………………………………………………………………
CCBRT imejikita kutoa huduma za tiba zinazofikiwa na wagonjwa wanazimudu, tiba vora na hali kadhalika kuzia ulemavu na kukuza kujumuishwa kwake nchini Tanzania. Moja ya tukio kubwa katika mkutano huo ilikuwa ni kukuza uelewa kuhusu umuhimu wa kutambua mapema, kutafuta tiba na na kufuatilia tiba yote ya miguu iliyopinda.
Mguu uliopinda ni ulemavu unaosababisha ama mguu mmoja ay miguu yote kupinda. Mguu unaoathirika unasababisha sehemu ya unyayo kubinuka kuelekea ndani kuanzia katika kifundo au kutembelea pande za miguu badala ya unyayo. Hata hivyo utambuzi wa mapema pamoja na tiba katika umri mdogo, huwafanya watoto waliozaliwa na na mguu uliopinda kuweza kutembea na kushiriki ipasavyo katika shughuli za kijamii na kiuchumi ndani ya jamii zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Usimamizi wa masuala ya Kiserikali wa Tigo, Sylvia Balwire alisema kuwa Tigo imejikita kurudisha kwa jamii ambamo inaendesha shughuli zake kupitia mikakati wake wa kuwajibika kwa jamii. “Tuliona kuna haja ya kusaidia katika hili kwa sababu CCBRT inahudumia maskini walioko pembezoni ndani ya jamii na inajaribu kuondoa vikwazo vingi kadiri iwezekanavyo ili kuwawezesha watu kutafuta tiba. Jamii itaikumbuka CCBRT daima kutokanana mkakati wake huu wa kuwasaidia watu walio na ulemavu na kuwapatia fursa ya kutibiwa kwa gharama nafuu. Inatakiwa mtu kuwa na moyo wa ziada kutoa huduma ambayo CCBRT inatoa kwa jamii.
Zaidi ya watoto 1,509 walishanufaika na upasuaji huu unaobadili maisha kutoka CCBRT katika kipindi cha zaidi ya miaka sita iliyopita. Haya ni mafanikio ambayo yanatufanya sisi sote tuliopo Tigo tunajivuania sana. Kupitia matibabu ya watu wanaoishi na ulemavu, Tigo na CCBRT wanaweka chapa ya kudumu katika ustawi wa watu binafsi, familia na jamii nchini Tanzania.
“Katika kuadhimisha Siku wa Miguu Iliyopinda duniani kwa mwaka huu na kama sehemu ya kujitoa kwetu kukuza ustawi wa jamii tunatoa msaada wa shilingi milioni 110 kwa CCBRT kwa ajili ya kusaidia matibabu ya miguu iliyopinda katika hospitali yake. Msaada huu kwa matibabu ya miguu iliyopinda ni kielelezo kwamba Tigo inaendelea kujikita katika kusaidia utoaji wa huduma za afya katika CCBRT na nchini kwa ujumla.
No comments :
Post a Comment