Saturday, June 3, 2017

MASAUNI AZINDUA MPANGO WA KUWASAIDIA WAKIMBIZI NA NCHI ZINAZOHIFADHI WAKIMBIZI LEO JIJINI DAR ES SALAAM


MASA1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke.  
MASA2
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) 
MASA3
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi  Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo.
MASA4
Sehemu ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini  pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
MASA5
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari  wakati wa uzinduzi wa  Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
MASA6
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments :

Post a Comment