Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Sukuhu Hassan, (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, huku Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, mara baada ya kufungua rasmi semina ya siku mbili kwa wastaafu watarajiwa kutoka wilaya zote saba za mkoa wa Mwana leo Juni 3, 2017. Semina hiyo inayolenga kuwanadaa wastaafu watarajiwa, imetayarishwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF |
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ameupongeza Mfuko
wa Pensheni wa PSPF, kwa hatua yake ya kuwataayarisha watumishi wa Umma wanaokaribia
kustaafu kwa kuwapatia semina ya mafunzo ili wastaafu kwa amani.
Akifungua
rasmi semina ya siku mbili kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na PSPF kwenye
ukumnbi wa chuo cha Watumishi wa BoT jijini Mwanza leo Juni 3, 2017, Makamu wa
rais Mama Samia Suuhu Hassan, (pichani juu), alisema, “Rais
amependezwa sana na jitihada zenu za leo za kuhakikisha mnawatayarisha wastaafu
wetu watarajiwa, na amesema nay eye asingekuwa rais basi hapana shaka kuwa nae
leo angekuwa miongoni mwa wanufaika wa semina hii, hongereni sana kwa kubuni
wazo hili.” Alisema mama Samia.
Kauli
mbiu ya semina hiyo ni “Mafao ni Mtaji wa Uwekezaji Sahihi” na kwa mujibu wa
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, kwa mwaka wa 2017/018 Mfuko
unatarajia kulipa Wastaafu 9,552 Mafao
yanayofikia Shilingi Trilioni 1.3.
Aidha
Rais Magufuli amesema katika salamu zake zilizosomwa na Makamu wa Rais kwa
washiriki wa semina hiyo kuwa, anaipongeza PSPF kwa kuendelea kumuunga mkono
katika jitihada zake za kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda ifikapo
mwaka 2025 na kuwa asilimia 40 ya ajira itatoka kwenye viwanda hivi.
Katika
semina hiyo, pamoja na mambo mengine,washiriki wamepatiwa mafunzo ya uanzishaji
viwanda vidogo vidogo toka kwa maafisa wa Shirika la Viwanda Vidogo vidogo
nchini SIDO.
Aidha
Makamu wa Rais kwa upande wake alisema,
amefurahishwa na ubunifu huo na kuitaka mifuko mingine kuiga mfano huo kwani
una manufaa makubwa katika kuwandaa watumishi wa umma wanapojiandaa kustaafu
ili kuondoa hofu ya namna ya kuishi baada ya utumishi wa umma.
“Lakini
niungane na Naibu waziri wa Fedha na Mipango, aliysema ninyi sio wastaafu
watarajiwa bali ni wawekezaji watarajiwa, na hivyo nawaasa, fedha mtakazopata
mzitumie kwa malengo yatakayoboresha maisha yenu, lakini pia akina baba nao
watumie fedha hizo kuanzisha miradi mipya na sio kuongeza wake.” Alsiema Makamu
wa Rais.
Akieleza
zaidi, Makamu wa Rais amewataka washiriki hao kubadili mfumo wa matumizi ya
fedha ili kueldana na hali halisi, ikiwa ni pamoja na kutotumia fedha ovyo kwa
matumizi makubwa yasiyo na manufaa.
Naye
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amewatia shime wastaafu
hao watarajiwa kuwa wachangamkie fursa mbalimbali zinazojitokeza kutokana na
semina hii ambapo wadau wa PSPF, kama vile taasisi za kifedha zimetoa elimu ya
huduma wazitoazo ambazo pia zinaweza kuwa na manufaa kwao.
Lakini
ninyi sio wastaafu watarajiwa ninyi ni wastaafu wawekezaji hivyo mmestaafu
utumishi wa umma na hamjastaafu kazi.” Alsiema Dkt. Kijaji.
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (pichani juu), akitoa taarifa yake alisema, “Nchi yetu
ina jumla ya Mifuko ya Pensheni mitano kwa Tanzania bara na mmoja kwa Tanzania
Visiwani, pamoja na idadi hii ya Mifuko, PSPF ndio Mfuko wenye idadi kubwa ya
wastaafu kwa mwaka na pia daftari kubwa la malipo ya pensheni kila mwezi.”
Alifafanua na kuongeza
“PSPF
inahudumia wanachama 403,605 na wastaafu wategemezi 62,892 ambao kwa kiasi
nkikubwa ni watumishi wa umma wakiwemo walimu, askari polisi, askari magereza,
aidha kwa upande wa uchangiaji wa Hiari Mfuko una wanachama 86,900 na hii ni
kuhakikisha Mfuko unatekeleza kwa vitendo juhudi za serikali za kuhakikisha
kuwa wananchi wengi zaidi wanafaidika na mfumo wa hifadhi ya jamii nchini.
Furaha ya hotuba nzuri
Furaha ya hotuba nzuri
Kutoka kushoto ni ni Meneja Pensheni za
Wastaafu wa PSPF, Bw. Mohammed Salim, Meneja Mipango na Utafiti, wa
PSPF, Bw. Luseshelo Njeje, na Mkurugenzi wa Masoko Mfuko wa UTT-AMIS,
Bw. Daudi Mbaga, wakifurahia jambo
Mshiriki wa semina akionyesha furaha yake kufuatia hotuba murua ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
Washiriki wakifuatilia semina
Huyu ni mmoja wa wastaafu ambaye sasa anafaidika na Mafao ya PSPF, akionyesha shukrani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Sukuhu Hassan, akipewa maelezo ya utangulizi kuhusu semina kwa
wastaafu watarajiwa toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.
Adam Mayingu, ambapo baadaye Mama Samia lifungua rasmi semina hiyo iliyofanyika
ukumbi wa chuo cha watumishi wa BoT, jijini Mwanza leo Juni 3, 2017. Zaidi ya
wastaafu watarajiwa 450 wanashiriki semina hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe. John Mongela akiongea
Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza nao walikuwepo
Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, amakamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais, akisindikizwa na Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Kijaji, Mkurugenzi Mkuu Mayingu, na
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Mongela
Makamu
wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, (wapili kulia), akisalimiana na Kaimu
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji, wakati
akiwasili ukumbi wa chuo cha watumishi wa BoT jijini Mwanza leo Juni 3, 2017
kufungua rasmi semina kwa wastaafu watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko huo na
kuwaleta pamoja washiriki zaidi ya 450n kutoka wilaya zote saba za mkoa wa
Mwanza. Anayeshuhudia wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam
Mayingu.
Sehemu ya washiriki wa semina
Mkurugenzi wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo,
(kushoto) ambaye anasimamia Mipango na Uwekezaji na Bi. Neema Muro
anayeshughulikia Uendeshaji wakifuatilia semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa
utulivu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na wasemaji wakionhozwa na Makamu
wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
No comments :
Post a Comment