Mwakilishi wa Taasisi ya Wel tel Story
,watayarishaji wa Mradi wa Shujaaz,Alan Lucky akizungumza na waandishi
wa habari (hawapo pichani ) kuhusu kufunguliwa kwa kijiji cha Shujaaz
katika Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki maarufu kama East Africa
Cup 2017 yanayofanyika katika shule ya Sekondari Moshi Ufundi .
Baadhi ya Wageni wakijiandikisha kabla
ya kuingia katika kijiji hicho ambako kumekuwa kukitolewa mafunzo
mbalimbali hasa ya Kilimo .
Mratibu wa Tafiti wa Mradi wa Shujaaz,Winnie Nyato akitoa tiketi kwa mmoja wa watoto waliotembelea kijiji cha Shujaaz .
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma
,Mohamed Kombo anayejishughulisha na Kilimo cha matunda akizungumza na
vijana waliofika katika kijiji cha Shujaaz kuona namna gani wanaweza
kuhamasika na kuingia katika shghuli za Kilimo.
Mjasiliamali Khalfa Muslim akitoa elimu
jinsi ya kutengeneza mchanganiko wa Matunda kwa vijana waliotembelea
kijiji cha Shujaaz kilichopo katka viwanja vya Shule ya sekondari Moshi
Ufundi yanapofanyika mashindano ya East Africa Cup 2017.
Mjasiliamali Holo Bukombe akionesha
bidhaa mbalimbali ambazo amekuwa akiziweka katika vifungashio maalumu na
kuongeza thamani ya bidhaa husika.
Afisa Masoko wa kamuni ya YARA Ltd
,Linda Byaba akitoa elimu kuhusu kilimo bora na chenye tija na jinsi ya
kuongeza thamani ya mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya
Mbolea kwa Mwakilishi wa taasisi ya Wel tel Story ,Alan Lucky.
Muonekano wa kijiji cha Shujaaz
kilichopo katika Shule ya Sekondari Moshi Ufundi ambako elimu mbalimbali
hususani za Kilimo pamoja na michez kwa vijana imekuwa ikitolewa.
Baadhi ya watoto wakishindana michezo mbalimbali (Games) katika kijiji cha Shujaaz.
Vijana wengine wamepaa fursa ya kucheza mchezo wa mitupo ndani ya kijiji hicho.
Vijana wengine walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hasa vya kuimba na kucheza na kuambulia zawadi kutoka Shujaaz.
Na Dixon Busagaga wa Glob ya Jami ,Kanda ya Kaskazini.
No comments :
Post a Comment