Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Zanzibar, Nagma Giga akimkabidhi komputa Katibu wa Wazazi Mkoa wa Kaskazini Bi.Zaituni Bushiri Ussi. |
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Wazazi CCM Zanzibar, Nagma Giga akizungumza na Watendaji na viongozi wa
jumuiya hiyo wa ngazi za Mikoa na Wilaya mara baada ya kuwakabidhi
komputa.
Baadhi ya Komputa zilizokabidhiwa kwa Makatibu wa Mikoa na Wilaya jumuiya ya Wazazi za Zanzibar.
…………………….
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
JUMUIYA ya Wazazi ya CCM Zanzibar
imewataka watendaji wake wa ngazi mbali mbali za jumuiya hiyo kuwa
waadilifu wakati wa kuchuja majina ya wagombea wanaowania nafasi mbali
mbali za uongozi kupitia uchaguzi unaoendelea ndani ya chama na jumuiya
zake.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bi.Nagma Giga wakati akikabidhi vitendea
kazi ambavyo ni komputa na priter kwa Mikoa na Wilaya nane za jumuiya
hiyo huko katika Afisi Kuu ya Wazazi Mpirani Kikwajuni Unguja.
Alisema watendaji wa ngazi za
mikoa na wilaya za jumuiya hiyo ndio wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo
kwa ngazi mbali mbali za jumuiya hivyo wakati wa kuchuja wagombea ni
lazima waweke kando urafiki na undugu na wawapitishe viongozi wenye sifa
na uzalendo wa kukisaidia chama kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.
“Mafanikio tuliyonayo ndani ya
jumuiya yrtu yanatokana na juhudi zenu za kiutendaji hivyo nakupongezeni
sana na muendelee na kasi hiyo hiyo hadi tupate viongozi imara
watakaotetea maslahi ya CCM mwaka 2020”,.alisema Giga.
Aidha aliwasisitiza viongozi hao
kuhakikisha wanatunza vizuri vifaa walivyopewa na kuvitumia kwa malengo
yaliyokusudiwa ili kurahisisha shughuli za kiutendaji za jumuiya.
Akitoa neno la shukrani Katibu wa
Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bi.Zaituni Bushiri Ussi aliahidi kuwa
vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya kuharakisha maendeleo ya taasisi
katika harakati za kiutendaji.
Naibu Katibu Mkuu huyo ametoa
Komputa nane zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa Mikoa na
Wilaya zote za Jumuiya hiyo Zanzibar ili kukamilisha ahadi alizotoa
katika ziara zake visiwani humo.
Komputa hizo zimetolewa kwa Mkoa
Kaskazini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkoa
wa Kusini Pemba, Wilaya ya Kaskazini “A”, Wilaya ya Dimani, Wilaya ya
Amani na Wilaya ya Amani.
No comments :
Post a Comment