Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (kushoto) na Balozi
wa Umoja wa Ulaya nchini Mhe.Roeland Van De Geer (kulia) wakifunua
kitambaa kuonyesha jiwe la msingi linaashiriwa kufunguliwa kwa Kituo
cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii kilichopo katika jengo la Old
Boma leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao (mwenye mtandio)
akiwa katika picha na wageni waliohudhuria hafla ya ya kufungua kituo
cha Urithi wa Ubunifu Majengo kilichopo katika jengo la Old Boma na
Utalii leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini
Mhe.Roeland Van De Geer akiongea wakati wa hafla ya kufungua kituo cha
Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii katika jengo la Old Boma leo Jijini
Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe.Isaya Mwita akiongea na wageni (hawapo katika picha) wakati
wa hafla ya kufungua Kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii
kilichopo katika jengo la Old Boma leo Jijini Dare s Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao akitoa hotuba kwa
niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe katika hafla
ya kufungua kituo cha Urithi wa Ubunifu Majengo na Utalii kilichopo
katika jengo la Old Boma leo Jijini Dar es Salaam.
………………….
Na Lorietha Laurence- WHUSM.
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao ameupongeza Uongozi
wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kulifanya jengo la Old Boma
kuwa Kituo cha Urithi wa Ubunifu wa Majengo na Utalii (DARCHI).
Akizungumza katika hafla ya
kufungua kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Harrison Mwakyembe, Millao
alisema hatua hiyo inadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kuwa
utamaduni wa Mtanzania unadumishwa na kukuzwa.
“Ni dhahiri kuwa wananchi
wataweza kufahamu umuhimu wa kutunza na kuhifadhi majengo ya kale
kutokana na elimu watakayoipata kupitia kituo hiki katika kukuza
utamaduni ” alisema Millao.
Aidha alitoa wito kwa kwa Jumuiya
ya Wasanifu Majengo Tanzania kuendelea kushirikiana na Taasisi za ndani
na nje ya nchi katika kutekeleza mipango ya kutunza majengo na sehemu za
kale ili kuhifadhi historia na utamaduni wa Mtanzania.
Pia amezitaka Mamlaka za Serikali
za Mitaa katika Jiji la Dar es Salaam kusimamia sheria kwa kushughulia
kero mbalimbali zinazotokana na udhaifu wa sheria za kuendeleza majengo
ya kale.
Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Dar
es Salaam Bw.Isaya Mwita ameeleza kuwa kufunguliwa kwa kituo hiko ni
fursa ya kukuza pato la uchumi wa nchi kupitia mapato ya watalii
watakaokitembelea.
“Tayari tumeweka mipango
mbalimbali ya kuhakikisha Jiji letu la Dar es Salaam linakuwa sehemu ya
Utalii kwa kutoa mafunzo kwa madereva Taxii ambao wanahusika katika
kuwasafirisha watalii ili wawe na uelewa zaidi kuhusu kituo hiki ”
alisema Mstahiki Meya Bw.Mwita.
Kwa Upande wake Balozi wa Umoja wa
Ulaya Nchini Mhe.Roeland Van De Geer amesema ofisi yake iko tayari
kushirikiana kwa karibu na Jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla
katika kuleta maendeleo.
No comments :
Post a Comment