Global TV Online Yatoa Msaada Kwa Watoto Yatima Magomeni
Kiroba
cha mchele kikishushwa kwenye gari la Global Tv Online waliotoa msaada
huo kwenye Kituo cha Kulelea Yatima, Umra, kilichopo Magomeni,jijini Dar
es Salaam kwa ajili ya Sikukuu ya Iddi kesho.
Global Tv Online inayomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers,
leo imetoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwemo chakula, vinywaji na
sababu kwa watoto yatima wa Kituo cha Umra kilichopo Magomeni jijini Dar
es Salaam.
Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alikabidhi
mchele, unga na sukari pamoja na vinywaji mbalimbali pia sabuni kwa
ajili ya sikukuu ya Iddi inayotarajiwa kusherehekewa kesho na aliwatakia
sikukuu njema watoto hao.
No comments :
Post a Comment